Pata taarifa kuu

Zimwi la ghasia za uchaguzi latanda Zimbabwe

Mwanaharakati wa upinzani alidungwa kisu, makumi ya watu kukamatwa na wengine kutishwa: kampeni iliyojaa matukio ya uchaguzi mdogo wa wabunge na wa serikali za mitaa nchini Zimbabwe, wenye vigingi vichache, inazua hofu ya kurejea kwa zimwi la zamani la ghasia za uchaguzi kabla ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwaka ujao.

Mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.
Mji mkuu wa Zimbabwe, Harare. Jekesai NJIKIZANA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita ya kampeni, chama kikuu cha upinzani cha CCC kimevutia umati wa watu waliovalia mavazi ya njano kwenye mikutano ya hadhara. Chini ya ulinzi mkali, mikusanyiko mingi kati ya hii ilipigwa marufuku na mamlaka.

Lakini licha ya ukandamizaji huo, chama cha mpinzani Nelson Chamisa kiliibuka kidedea katika uchaguzi huo mwishoni mwa juma lililopita. CCC haikuweza kuwapindua walio wengi katika chaguzi hizi ndogo, lakini ilishinda viti 19 vya ziada bungeni.

Polisi ya Zimbabwe, ambayo kwa kawaida haipendi kuukosoa utawala, ilisema wafuasi wa Rais Emmerson Mnangagwa na chama chake cha ZANU-PF walihusika na matukio hayo wakati wa kampeni. Washukiwa watano walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji.

Zimbabwe ina historia ndefu ya ghasia za uchaguzi. Katika uchaguzi mkuu wa kwanza baada ya Mugabe mwaka 2018, ghasia zilisababisha vifo vya takriban watu sita. Baada ya kuchaguliwa, Emmerson Mnangagwa alikuwa ameahidi kufungua ukurasa wa miaka 37 ya utawala uliofanyika kwa mkono wa chuma na Robert Mugabe. Lakini mara kwa mara anashutumiwa kwa kutaka kunyamazisha sauti yoyote pinzani.

Zimbabwe: Upinzani unatumai kuongoza serikali ijayo

Wakati uchaguzi ukikaribia wikendi iliyopita, wanachama wa upinzani walikashifu vitisho kutoka kwa polisi. Emmerson Mnangagwa aliahidi kusitisha mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojaribu kuzuia nchi hiyo iliyoathirika kiuchumi kutokana na kukumbwa na janga la njaa.

"Tunaweza kufanya bila mashirika yasiyo ya kiserikali. Nitayafanya yatoweke katika nchi hii, nitayafukuza," aliahidi. Mswada wa marekebisho ya sheria unazingatiwa Bungeni.

Kupiga marufuku vyama ni mbinu ambayo ilitumiwa na Mugabe mwaka 2008, ili asishindwi katika uchaguzi. Aliyawashutumu kwa kuwahonga watu chakula ili wapigie kura upinzani.

"Tunahofia kwamba sehemu ya watu watajikuta wametengwa," Jestina Mukoko, mkurugenzi wa Mradi wa Amani wa Zimbabwe (ZPP), shirika la kutetea haki za binadamu, ameliiambia shirika la habari la AFP.

"Nafasi ya kidemokrasia inapungua na ikiwa marekebisho yatapita, itakuwa mbaya zaidi," ameongeza mwanaharakati huyu ambaye tayari alifungwa jela mara kadhaa. Alitekwa nyara mwezi Desemba 2008, anasema alihojiwa na kuteswa kwa siku kadhaa na wanaodaiwa kuwa maafisa wa idara ya ujasusi nchini Zimbabwe.

Kulingana na Blessing Vava, mkurugenzi wa kundi linalounga mkono demokrasia la Crisis Coalition, Bw Mnangagwa anataka "kuanzisha mfumo wa chama kimoja na udikteta ambapo serikali haiwajibiki".

Zaidi ya euro milioni 720 za misaada ya kibinadamu pia hupitia mashirika yasiyo ya kiserikali kila mwaka. Kupigwa marufuku kwa mashirika haya kunaweza kusababisha kupunguzwa kwa misaada inayotolewa kwa nchi iliyo katika mzozo wa kiuchumi kwa zaidi ya miaka ishirini na ambapo kila kitu kinakosekana, chakula, umeme, mafuta.

Misaada ya kimataifa ni mapato ya tatu kwa ukubwa baada ya mauzo ya nje na fedha kutoka nje ya nchi, kulingana na ŕipoti ya hivi majuzi ya wataalam wa maendeleo wa Zimbabwe, ambayo inatokana na takwimu kutoka Benki Kuu ya Zimbabwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.