Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Zimbabwe kupiga kura katika hali ya ukandamizaji

Takriban wapiga kura milioni sita wameitwa kupiga kura Jumatano Agosti 23 kwa uchaguzi wa urais, wa wabunge na wa serikali za mitaa, huku majina mawili yakijitokeza kati ya wagombea 11 wa kiti cha urais: Emmerson Mnangagwa, rais anayemaliza muda wake wake na kiongozi wa upinzani, Nelson Chamisa, mwanasheria na mchungaji. 

Mamlaka imeongeza idadi ya kikosi chake cha ukandamizaji kabla ya uchaguzi. Hapa, maafisa wa polisi wakizingira lori likiwa limbebeba wafuasi wa upinzani, kabla ya kufikishwa mahakamani, wakishtakiwa kwa kuzorotesha shughuli za uchukuzi, mjini Harare, Agosti 17, 2023.
Mamlaka imeongeza idadi ya kikosi chake cha ukandamizaji kabla ya uchaguzi. Hapa, maafisa wa polisi wakizingira lori likiwa limbebeba wafuasi wa upinzani, kabla ya kufikishwa mahakamani, wakishtakiwa kwa kuzorotesha shughuli za uchukuzi, mjini Harare, Agosti 17, 2023. © Tsvangirayi Mukwazhi / AP
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu unafanyika katika hali ya wasiwasi: upinzani unashutumu kuongezeka kwa ukandamizaji katika nchi, ambayo inakabiliwa na umaskini na mfumuko wa bei unaozidi kushika kasi.

Uchaguzi wa urais ni sawa na mechi ya marudiano kati ya wagombea wawili wakuu: walipambana mwaka wa 2018, wakati wa uchaguzi wa kwanza bila Robert Mugabe, ambaye aliongoza nchi hii kwa mkono wa chuma kwa miaka 30.

Rais anayemaliza muda wake Emmerson Mnangagwa wa chama tawala cha Zanu-PF, hakupendekeza mpango wa uchaguzi: anabainisha kwamba rekodi ya chama chake inatosha. Hii inalenga katika miundombinu: ujenzi wa shule, barabara kuu na madaraja. Ushahidi mwingi kwamba rais anatimiza ahadi zake,kulingana na wafuasi wake.

Lakini tuhuma za ufisadi zimechafua taswira ya miradi hii ya kitaifa, hali iliyosababisha pia Marekani kuiwekea vikwazo Zimbabwe. Haya yamebainishwa na Rais anayemaliza muda wake Emmerson Mnangagwa, aliyepewa jina la utani la "mamba", kuelezea asili ya matatizo ya kiuchumi ya nchi hiyo.

Kuhusu Nelson Chamisa, mpinzani wake ambaye tayari alishindwa kwa pointi ndogo mwaka wa 2018, alizindua programu yake wiki mbili tu kabla ya uchaguzi: wengine wanamkosoa kwa kukosa maono. Chama chake, Muungano wa Wananchi kwa ajili ya Mabadiliko - au "C mara tatu" - kinashutumu vitisho na kupigwa marufuku kwa mikutano yake na mamlaka: Agosti 3, mwanaharakati wa CCC alipigwa mawe hadi kufa na watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa Zanu-PF.

Human Rights Watch tayari imetabiri "mchakato wa uchaguzi wenye dosari kubwa".

Rais anachaguliwa kwa wingi wa kura. Raundi ya pili inapangwa tu ikiwa hakuna mgombea atashinda 50% ya kura kujumuisha moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.