Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi Zimbabwe: Waangalizi wa ndani walaani udanganyifu

Nchini Zimbabwe, wapiga kura milioni sita na nusu wameitwa kuchagua rais wao, wabunge wao na madiwani wao, Jumatano hii, Agosti 23, katika mazingira ya mgogoro wa kiuchumi na rekodi ya mfumuko wa bei. Wagombea wawili wakuu wa urais ni mkuu wa nchi anayemaliza muda wake Emmerson Mnangagwa, 80, na Nelson Chamisa, wakili na mchungaji mwenye umri wa miaka 45.

Wapiga kura wakiwa wamejipanga nje ya kituo cha kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi wa Zimbabwe mjini Harare, Jumatano, Agosti 23, 2023.
Wapiga kura wakiwa wamejipanga nje ya kituo cha kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi wa Zimbabwe mjini Harare, Jumatano, Agosti 23, 2023. AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu wa urais ni sawa na mechi ya marudiano kati ya wagombea wawili wakuu: walipambana mwaka wa 2018, wakati wa uchaguzi wa kwanza bila Robert Mugabe, ambaye aliongoza nchi hii kwa mkono wa chuma kwa miaka 30.

Rais anayemaliza muda wake Emmerson Mnangagwa wa chama tawala cha Zanu-PF, hakupendekeza mpango wa uchaguzi: anabainisha kwamba rekodi ya chama chake inatosha. Hii inalenga katika miundombinu: ujenzi wa shule, barabara kuu na madaraja. Ushahidi mwingi kwamba rais anatimiza ahadi zake,kulingana na wafuasi wake.

Kulikuwa na mistari mirefu nje ya vituo vya kupigia kura, lakini vingi vya vituo hivi vilifunguliwa kwa kuchelewa sana, na hii inaweza kuzuia baadhi ya wapiga kura kupiga kura kabla ya giza kuingia, kulingana na waangalizi wa ndani walioidhinishwa.

Waangalizi hawa pia wamegundua mbinu za vitisho vya kuwatisha wapiga kura: kuondoka kwenye uchaguzi ambapo mtu anahitaji nambari ya kitambulisho na nambari ya simu.

"Kuna shirika linaitwa Forever Associates Zimbabwe ambalo lina uhusiano na chama cha ZANU-PF na ambalo limeweka meza kwenye milango ya vituo vya kupigia kura, kutekeleza kile wanachokiita uchunguzi wa matokeo ya uchaguzi," anathibitisha Jestina Mukoko, wa timu hii ya waangalizi wa ndani kutoka shirika la Zimbabwe Peace Project, ambalo yeye ni mkurugenzi wake.

"Tunachoogopa, anasema, ni kwamba inaleta hofu kwa watu, na inawatisha wapiga kura, kushawishi kura zao, baada ya kumtaka kila mpiga kura anapomalizi kupiga kura atoe nambari zake za kitambulisho na nambari yake ya simu. "

Sababu yetu nyingine ya wasiwasi ni kwamba vituo vingi vya kupigia kura havikufunguliwa kwa wakati na vingine vimechelewa sana. Inayomaanisha kuwa watu watalazimika kupiga kura usiku, na inaweza isiwatie moyo sana kuwa nje usiku ili kupiga kura.

Haya yote ni baada ya kampeni ambayo tayari imedhihirishwa na ukandamizaji wa upinzani, kwa upande wa serikali ya rais anayemaliza muda wake Emmerson Mnangagwa, ambaye kwa hiyo anawania muhula wa pili katika uongozi wa Zimbabwe.

Wafuasi wa mpinzani wake mkuu, Nelson Chamissa, wamefungwa. Mikutano mia moja imepigwa marufuku. Mtandao pia ulizimwa na vibali vilikataliwa kwa wanahabari wengi wa kigeni na waangalizi wa mashirika ya kiraia.

Kuna hofu kubwa ya udanganyifu wa kura, dosari tayari zimebainishwa kwenye orodha za wapiga kura.

Kama ukumbusho, Bw. Mnangagwa, ambaye hapo awali alimwondoa Robert Mugabe mamlakani, alishinda uchaguzi wa urais mwaka wa 2018 dhidi ya Bw. Chamisa. Na alikandamiza maandamano yaliyofuata, na kuua watu sita

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.