Pata taarifa kuu

Ombi la Algiers kujiunga na muungano wa BRICS katika mkutano wake wa 15

Mnamo Novemba 2022, Algeria iliwasilisha ombi rasmi la kujiunga na kundi la BRICS. Kundi ambalo, kulingana na Algiers, linashiriki katika kusawazisha uhusiano wa kimataifa. Kwa Algeria, nchi zinazounda BRICS ndizo moyo wa kutofungamana na upande wowote. Nchi ambazo zinapamana kwa minajili ya ulimwengu wa nchi nyingi.

Mkutano wa 15 wa kilele wa BRICS unaanza mjini Johannesburg mnamo Agosti 22, 2023.
Mkutano wa 15 wa kilele wa BRICS unaanza mjini Johannesburg mnamo Agosti 22, 2023. AFP - GIANLUIGI GUERCIA
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Algiers, Fayçal Métaoui

Nchi inayoandaa mkutano wa BRICS, Afrika Kusini, inaunga mkono uanachama wa Algeria kwa kundi hili, kama vile China na Urusi. India na Brazil bado hazijazungumza juu ya suala hilo.

Rais Abdelmadjid Tebboune alifanya ziara rasmi huko Moscow na Beijing, ambapo alihakikishiwa kuungwa mkono na nchi hizi mbili kwa kujiunga na kundi hilo. Tebboune pia alitangaza kwamba Dilma Rousseff, rais wa zamani wa Brazil na mkurugenzi wa sasa wa benki ya BRICS, alisema kuwa Algeria ni muhimu kwa kundi hili la kiuchumi.

Mnamo Julai 2023, Algeria iliomba kujiunga na Benki Mpya ya Maendeleo ya BRICS, na mchango wa awali wa kifedha wa dola bilioni moja na nusu.

Ikiwa na deni kupita kiasi na kuandamwa na ukosefu wa kudumu wa fedha za kigeni, Argentina pia inapenda kujiunga katika mmungano wa BRICS ili, hasa, kupata ufikiaji wa benki mpya ya maendeleo, tawi la kifedha la kambi ya nchi zenye nguvu zinazoibuka, anaripoti mwandishi wetu huko Buenos Aires, Théo Conscience. Kwa nchi hii, ufikiaji wa benki hii "unamaanisha ufikiaji wa moja kwa moja kwa chanzo cha mtaji wa kimataifa na viwango vya chini vya riba ambavyo vinaweza kuwa muhimu kwa uwekezaji nchini Argentina", anaelezea Bruno de Conti, profesa wa uchumi wa kimataifa katika Chuo Kikuu cha Condominas.

Lakini kukosekana kwa utulivu wa serikali ya Argentina ni kikwazo kikubwa, hasa kwani uungaji mkono wa Brazil na China kwa Argentina kugombea kujiunga katika BRICS, ulipooza siku ya Jumapili na matokeo ya kura ya mchujo katika uchaguzi wa urais, yaliyompa ushindi wa kushangaza Javier Milei ambaye yuko "karibu na Marekani".

Suala la kuachana na dola

Suala jingine linaweza pia kuathiri uchaguzi wa wanachama wapya: nia ya kuharakisha uondoaji wa dola, wakati BRICS wanataka kupunguza utegemezi wao kwa noti za kijani kibichi (dola). Daniel Bradlow, profesa katika Chuo Kikuu cha Pretoria anasema "nchi za BRICS zinatumia kwa mfano yuan katika biashara zao, ni vigumu kwa nchi zingine kutumia sarafu hizi. Kwa mtazamo wa biashara, kuna uwezekano wa kuendeleza hili. »

Mataifa mengine, hasa kutoka Ghuba, kama vile Saudi Arabia na Falme za Kiarabu, au nchi zilizo chini ya vikwazo kama vile Iran, pia zinataka kujiunga na mungano huu wa BRICS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.