Pata taarifa kuu

Swali gumu la upanuzi wa muungano wa BRICS

Afrika Kusini ni mwenyeji wa mkutano wa kilele wa BRICS kuanzia Agosti 22 hadi 24 katika kituo chake cha mikutano mjini Johannesburg. Mkutano maalum wa kilele, wa kwanza wa ana kwa ana tangu janga la UVIKO na kuanza kwa vita nchini Ukraine. Rais wa Urusi Vladimir Putin pia atafuata mkutano huo kwa njia ya video, hawezi kusafiri kutokana na kibali cha kukamatwa cha ICC.Β 

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva (katikati) alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa OR Tambo huko Ekurhuleni jijini Johannesburg, kabla ya mkutano wa kilele wa BRICKS, Agosti 21, 2023.
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva (katikati) alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa OR Tambo huko Ekurhuleni jijini Johannesburg, kabla ya mkutano wa kilele wa BRICKS, Agosti 21, 2023. AFP - RICARDO STUCKERT
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa masuala makuu yaliyopo mezani ni suala la upanuzi wa BRICS. Tangu kuongezwa kwa Afrika Kusini mwaka 2010, hakuna nchi mpya ambayo imejiunga na muungano huu. Hoja hii imekuwa ikijadiliwa katika miezi ya hivi karibuni, hasa katika ngazi ya mawaziri, na sasa Wakuu wa Nchi wataweza kujadili chaguo hili muhimu.

Wakati nchi kama China au Urusi zimefahamisha nia yao ya kujitanua, ili muungano huo uwe na uzito zaidi na uweze kulazimisha matamanio yake ya umoja wa pande nyingi, wanachama wengine kama India au Brazil, na rais wake Lula, kwa sasa wako waangalifu zaidi: "Tutajadili kujiunga kwa nchi mpya, na nina maoni kwamba nchi yoyote inaweza kujiunga, mradi iheshimu sheria ambazo tuko katika mchakato wa kuanzisha: kwa kuzingati ili, tutakubali maombi yao. "

Kwa sababu ni vigezo hivi vya kuingia hasa ndivyo ambavyo ni vigumu kuanzisha kati ya nchi tano. Waraka umetayarishwa na wakuu wa kidiplomasia, lakini lazima sasa ukubaliwe na wakuu watano wa nchi wanachama wa BRICS.

Kulingana na Afrika Kusini, nchi 23 zimekaribia rasmi muungano huo kwa uwezekano wa kugombea. Nia inayotokana na mabadiliko ya kijiografia na kisiasa, kulingana na Priyal Singh, mtafiti katika Taasisi ya Mafunzo ya Usalama (ISS): "Tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, kumekuwa na mvutano mkubwa wa kijiografia na kisiasa duniani, na hii inawafanya watu kuwa na wasiwasi sana katika nchi za kusini. Nadhani nchi nyingi zinatafuta kutabirika zaidi, na zinaweza tu kuipata kwa kuunganisha uzito na ushawishi wao ulimwenguni. Β»

Orodha hiyo iliyochapishwa na Pretoria inajumuisha nchi kadhaa barani Afrika, ambazo ni Algeria, Misri, Senegal, Nigeria, Ethiopia, na Morocco, ambazo wanadiplomasia hata hivyo wamekanusha kutoa ombi hilo. Kwa bara la Afrika, kuwa karibu na BRICKS pia ni njia ya kuimarisha uhusiano na China, ambayo inatawala kundi hilo, kulingana na Priyal Singh: "China ni mshirika nambari moja wa biashara kwa nchi nyingi za Afrika. Nadhani wengi wao wameelekeza macho yao kwa Beijing, hasa China inavyoendelea kukua, na kwa hivyo wanataka kukaribia mzunguko wake wa kisiasa na kiuchumi. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.