Pata taarifa kuu

Niger: ECOWAS iko 'tayari kuingilia kati' mara tu 'amri itakapotolewa'

Kikosi cha ECOWAS kiko "tayari kuingilia kati" nchini Niger mara tu viongozi wa nchi za Afrika Magharibi watakapotoa amri, amesema kamishna wa masuala ya kisiasa, amani na usalama wa jumuiya hiyo ya kikanda, Abdel - Fatau Musah.

Mkuu wa jeshi la ulinzi wa Ghana Seth Amoama (wa kwanza mstari wa 4 kulia) na Waziri wa Ulinzi wa Ghana Dominic Nitiwul (safu ya 1 katikati) wakipiga picha ya pamoja na wajumbe kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) wakati wa Mkutano usio kuwa wa kawaida wa ECOWAS mjini Accra, Ghana tarehe 17 Agosti 2023.
Mkuu wa jeshi la ulinzi wa Ghana Seth Amoama (wa kwanza mstari wa 4 kulia) na Waziri wa Ulinzi wa Ghana Dominic Nitiwul (safu ya 1 katikati) wakipiga picha ya pamoja na wajumbe kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) wakati wa Mkutano usio kuwa wa kawaida wa ECOWAS mjini Accra, Ghana tarehe 17 Agosti 2023. AFP - GERARD NARTEY
Matangazo ya kibiashara

"Tuko tayari kuingilia kati mara tu amri itakapotolewa. Siku ya kuingilia kati pia imepangwa na inajulikana", ametangaza afisa huyu baada ya mkutano wa wakuu wa majeshi ya Afrika Magharibi waliokutana tangu siku ya Alhamisi mjini Accra, nchini Ghana.

Wakuu wa majeshi ya ECOWAS waliamua juu ya mbinu za uingiliaji kati kijeshi kama njia ya mwisho ya kumrejesha madarakani rais mteule Mohamed Bazoum aliyetimuliwa mamlakani tangu Julai 26 na utawala mpya wa kijeshi huko Niamey. Lakini walisisitiza tena kwamba ECOWAS inaweka mbele njia ya mazungumzo.

Hata hivyo ECOWAS ilitangaza kutuma ujumbe "unaowezekana" wa kidiplomasia siku ya Jumamosi nchini Niger, wakati wajumbe wa awali kutoka jumuiya hiyo ya kikanda walishindwa kukutana na Jenerali Tiani, kiongozi mpya wa nchi hiyo.

"Tuko tayari kusuluhisha tatizo hilo kwa amani, lakini kunahitajika pande mbili kufikia suluhu," Musah amesema.

Lakini "sisi hatutakuwa wa kubisha mlango wakati hawataki kufungua," ameongeza, hata hivyo.

Ikiwa jeshi nchini Niger "linataka kuchukua njia ya amani ili kurejesha utaratibu wa kikatiba haraka iwezekanavyo, tuko tayari kuacha chaguo la kijeshi, kwa sababu sio chaguo letu tunalopendelea, lakini tunalazimika kufanya hivyo kwa sababu ya utawala usio na usawa, " amebainisha.

Kuhusu uingiliaji unaowezekana, "Nchi zote wanachama wa ECOWAS waliopo hapa leo wamejitolea kutoa wanajeshi, vifaa na uwezo unazohitajika kutekeleza azma hii," ofisa huyo amesema.

"Tumekubaliana na kufanyia kazi nini kitahitajika kwa ajili ya operesheni ii. Je, ni malengo gani ya kimkakati, vifaa vinavyohitajika na dhamira ya nchi wanachama," alisema.

Nchi zote za ECOWAS zimewakilishwa katika mkutano huu isipokuwa Cape Verde na Guinea-Bissau.

Kwa upande wa Guinea, Mali na Burkina Faso, zilisimamishwa kwenye bodi zinazosimamia ECOWAS kwa vile zao pia zimekuwa wakiongozwa na wanajeshi waliofanya mapinduzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.