Pata taarifa kuu

Mgogoro Niger: kwa nini Baraza la Amani na Usalama la AU halijatangaza msimamo wake

Vikosi vya usalama na ulii vimefanya msako wa kushtkiza kwenye nyumba za watu walio karibu na Rais Mohamed Bazoum, ambao bado wanazuiliwa na jeshi tangu mapinduzi ya Julai 26, na pia katika nyumba za wmaafisa wa serikali yake na wanachama wa chama chake. Msako huo ulifanyika usiku wa Alhamisi Agosti 17 kuamkia Ijumaa 18, 2023. 

Nembo ya Umoja wa Afrika, kwenye makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Nembo ya Umoja wa Afrika, kwenye makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Afrika unachelewa kutoa maoni yake kuhusu mgogoro wa Niger. Tangu mkutano wa Agosti 14 wa Baraza la Amani na Usalama la AU (PSC), taasisi hiyo ya bara bado haijachapisha taarifa yake ya mwisho kuhusu msimamo utakayopitishwa dhidi ya utawala wa kijeshi kutoka Baraza la kitaifa la ulinzi wa taifa (CNSP).

Kulingana na vyanzo vya kidiplomasia vya Afrika vilivyohojiwa na RFI, mijadala ilikuwa "ya wazi" lakini hasa "migumu", chaguo la kijeshi lililopendekezwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) halijaidhinishwa na nchi zote wanachama wa jumuiya hiyo.

Mwishoni mwa mkutano wao, nchi wanachama wa PSC ziliingia katika "utaratibu wa ukimya". Hii ina maana kwamba taarifa iliyosubiriwa kwa muda mrefu iliyopaswa kuashiria msimamo wa Umoja wa Afrika kuhusu vikwazo vya ECOWAS inaandaliwa na sekretarieti ya Baraza la Amani na Usalama la AU....

Kwa mujibu wa taarifa kutoka RFI, hati hiyo iliwasilishwa jana usiku kwa wanachama wa CPS, na wajibu kwa washiriki kutofichua maudhui yake. Kwa hivyo utaratibu huu wa ukimya.

Kabla ya kuchapishwa kwa taarifa hii kwa vyombo vya habari, uongozi wa PSC, ambao kwa sasa unashikiliwa na Burundi, ulitaka kuendelea na majadiliano na nchi wanachama wa ECOWAS kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya waasi nchini Niger.

Kwa sababu, kulingana na chanzo cha kidiplomasia cha Afrika kilichohojiwa na RFI, kinathibitisha kwamba wazo la kuingilia kijeshi lilikataliwa na wanachama wote wa Baraza, isipokuwa nchi za Afrika Magharibi ambazo ni Gambia, Senegal, Ghana na Nigeria.

Kuanzia sasa, tunasubiri kuona jinsi kila nchi wanachama wa Baraza itakavyoitikia taarifa hiyo ya siri. Ama kila mtu ataidhinisha, na inaweza kutolewa leo au kesho hivi punde, kulingana na chanzo chetu cha kidiplomasia. Aidha mjumbe ataleta pingamizi kwa nakala hii na Baraza liingie katika awamu mpya ya mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.