Pata taarifa kuu

Ecowas yasema iko tayari kuunda kikosi kuikabili Niger

Nairobi –  Wakuu wa Majeshi kutoka nchi za Jumuiya ya ECOWAS kutoka ukanda wa Afrika Magharibi, wanakutana leo na kesho jijini Accra nchini Ghana, kujadili mikakati ya kuivamia Niger, iwapo juhudi za kidiplomasia kumrejesha madaraka rais Mohammed Bazoum, zitagonga mwamba. 

Wakuu wa jeshi wanakutana nchini Ghana kujadili Niger
Wakuu wa jeshi wanakutana nchini Ghana kujadili Niger REUTERS - FRANCIS KOKOROKO
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu unakuja baada ya agizo la wakuu w anchi za ECOWAS kukutana wiki iliyopita jijini Abuja, na kuamua kuwa jeshi lianze maanndalizi ya kuingia Niger, iwapo jitahidi za kidiplomasia hazitofaulu. 

Wakati wanajeshi hao walikutana , wachambuzi wa usalama na siasa wanasema matumizi ya jeshi sio njia nzuri ya kutatua mzozo huu na badala yake, wanapendekeza mchakato wa kidiplomasia. 

Mpaka sasa, inaripotiwa kuwa kuna mgawanyiko kati ya nchi wanachama iwapo jeshi litumwe nchini Niger. Rais wa Cote Dvoire, Allsane Outtara tayari ameonesha utayari wa nchi yake kutuma kwa kikosi cha wanajeshi Elfu 1 kuunda kikosi cha ECOWAS. 

Hata hivyo, Maseneta nchini Nigeria, ambayo ndio Mwenyekiti wa sasa wa ECOWAS, wamepinga mpango wa jeshi la nchi yao kwenda Niger. 

Mataifa jirani ya Burkina Faso na Mali, ambayo pia yanaongozwa na jeshi, yameonya kuhusu matumizi ya nguvu, yakisema yatatuma vikosi vyake, kuisaidia Niger iwapo itavamiwa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.