Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

Video ya wanajeshi wa Senegal imedaiwa kuwa ya wale wa Niger wakijipanga kwa vita

Imechapishwa:

Wakati huu viongozi wa Jumuiya ya ECOWAS wakipanga uwezekano wa kuingilia kijeshi kwa kinachoendelea nchini Niger iwapo viongozi wa mapinduzi hawatamwachia huru rais Mohamed Bazoum na kurejesha mamlaka kwa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia, video iliibuka mtandaoni pamoja na madai kwamba inaonesha wanajeshi wa Niger wakijiandaa kwa makabiliano.

Video za kupotosha kuwa jeshi la Niger linajiaanda kwa vita iwapo itiingiliwa na Ecowas baada ya mapinduzi
Video za kupotosha kuwa jeshi la Niger linajiaanda kwa vita iwapo itiingiliwa na Ecowas baada ya mapinduzi © FMM
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo huu ni uongo. Video hiyo inaonesha gwaride la kijeshi la Senegal wakati wa sherehe za Siku ya Uhuru wa nchi hiyo mnamo Aprili 4, 2023.

Kwenye chapisho moja kwenye Instagram la Agosti 2, mwaka huu lilisoma hivi:Wanajeshi hawa wa Niger hawafanyi mzaha hata kidogo.

Kanda ya video inaonesha wanajeshi waliojihami wakiwa na bunduki na visu huku wakiimba nyimbo kama zile za vita. Wamezungukwa na kundi la watazamaji wanaoonekana kuvutiwa, baadhi yao wakirekodi tukio hilo kwa kutumia simu zao. Madai kama hayo pia yalisambazwa kwenye Facebook na TikTok.

Rais Bazoum anazuiliwa na jeshi, ambalo viongozi wake wametangaza kuwa wanashikilia mamlaka katika taifa hilo lisilo na utulivu la Afrika Magharibi.

Bendera ya Senegal in rangi ya kijani kibichi, manjano na nyekundu ikiwa na nyota katikati na inaonekana kuanzia mwanzo wa video hadi mwisho. Ukilinganisha na bendera ya Niger ambayo ina rangi ya chungwa, nyeupe na kijani kibichi ikiwa na nukta ya chungwa katikati.

Kumbuka pia msikilizaji mapinduzi ya Niger ni ya tatu katika wimbi la mapinduzi katika eneo la Sahel katika miaka mitatu iliyopita.

Vipindi vingine
  • 10:00
  • 10:00
  • 10:58
  • 10:01
  • 10:01
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.