Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Vyama saba vya kisiasa vinalenga kukiangusha chama tawala ANC

Nairobi – Muungano wa vyama saba vya kisiasa nchini Afrika Kusini umesaini makubaliano ya ushirikiano yanayolenga kukiondoa chama tawala cha ANC katika uchaguzi mkuu wa mwak wa 2024.

Vyama hivyo saba vinalenga kukishinda chama tawala cha ANC katika uchaguzi mkuu ujao
Vyama hivyo saba vinalenga kukishinda chama tawala cha ANC katika uchaguzi mkuu ujao © AP - Jerome Delay
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, iwapo vyama hivyo vitashinda katika uchaguzi huo, vitafanya kazi kwa pamoja na kugawana nyadhifa mbalimbali za wizara na viti vya ubunge.

Pia wanalenga kukizuia chama cha Economic Freedom Fighters cha Julius Malema kuingia madarakani.

Makubaliano hayo yanakuja wakati huu nchi hiyo ikikabiliana na hali mbaya ya uchumi, ufisadi, ukosefu wa ajira na mzozo wa nishati ambao haujawahi kutokea.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema ANC iko hatarini kupoteza wingi wake wa wabunge kwa mara ya kwanza tangu Afrika Kusini irejee kwenye demokrasia mwaka 1994.

Kambi hiyo mpya, hata hivyo, haijaamua ni nani atachaguliwa kuwa rais ikiwa itafaulu katika uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.