Pata taarifa kuu

Tangu mapinduzi, China yafuatilia kwa uangalifu maslahi yake ya kiuchumi nchini Niger

China ambayo ni mwekezaji wa pili nchini Niger baada ya Ufaransa na msambazaji wa kwanza wa bidhaa, imeonyesha tahadhari kubwa tangu mapinduzi ya kijeshi nchi Niger. Maslahi iliyo nayo nchini yamekua kwa kasi kwa miaka 15, kama inavyothibitishwa na kongamano la kwanza la uwekezaji kati ya China na Niger lililofanyika mnamo mwezi Aprili. Ikiwa vikwazo hivyo vitarefushwa, miradi kadhaa ya China itaathiriwa bila shaka.

Wafanyakazi wa Niger na China kwenye eneo la ujenzi wa bomba la mafuta, nchini Niger.
Wafanyakazi wa Niger na China kwenye eneo la ujenzi wa bomba la mafuta, nchini Niger. AFP - BOUREIMA HAMA
Matangazo ya kibiashara

"China hufanya kile inachosema na kusema kile inachofanya," alisema balozi wa nchi hiyo nchini Niger mnamo Julai 3 wakati wa hadhara katika Ikulu ya rais baada ya hapo alitangaza kwamba nchi yake itajenga kiwanda cha bidha za kilimo, madini na Hifadhi ya viwanda ya mali isiyohamishika. Lakini itafikiaje mpango wake huobaada ya wanajeshi kufanya mapinduzi na kuamua kushikilia madaraka. Wizara ya mambo ya nje ya China hadi sasa imejizuia kutoa wito wa suluhu la mazungumzo.

Kwa sasa katika sekta ya mafuta na madini, lakini pia katika sekta ya miundombinu, China itapoteza kwa sehemu kubwa ikiwa vikwazo vitachukuwa muda mrefu au kukosekana kwa utulivu.

Kwa mfano, ujenzi wa bwawa la Kandadji, ambalo linapaswa kuongeza uzalishaji wa umeme nchini kwa nusu, tayari umesitishwa na wafanyakazi wake kufukuzwa kazi. China Gezhouba Group, kampuni kubwa ya ujenzi ya China inayosimamia mradi huo, inaangazia vikwazo vya kifedha kufuatia maamuzi ya hivi punde yaliyochukuliwa na washirika wa Niger.

Petrochina, ambayo inajenga bomba la kuunganisha Niger na Benin zaidi ya kilomita 2,000, hadi sasa haijatoa tangazo lolote. Kabla ya mapinduzi, mradi huo ulipangwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2023.

Hakuna habari kwa sasa kutoka kwa kampuni ambazo zilikuwa za mwisho kuhitimisha makubaliano na Niger. Miongoni mwao, Sinopec, kampuni kubwa ya serikali ya China ya mafuta, tayari kuwekeza nchini, baada ya kampuni ya CNPC, ambayo inasimamia visma vya mafuta vya Agadez na kujenga kiwanda cha kusafishia cha Zinder. Lakini pia kampuni ya Kitaifa ya Uranium ya China ambayo inanuia kuzindua upya uzalishaji kwenye eneo la Somina kaskazini-magharibi mwa Agadez, uzalishaji ulikatizwa tangu 2015. Mkataba wa itifaki ulitiwa saini ili kufanya hivyo mwezi Juni mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.