Pata taarifa kuu

Mapinduzi Niger: Wakuu wa majeshi ya ECOWAS kukutana Agosti 12

RFI imepata habari kutoka duru za kuaminika kwamba mkutano wa Wakuu wa Majeshi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) umepangwa kufanyika Jumamosi hii, Agosti 12 huko Accra, nchini Ghana baada ya "kuanzishwa na kutumwa kwa kikosi cha kikanda" kwa lengo la kurejesha utawala wa kikatiba nchini Niger. 

Kamishna wa Masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), Balozi Abdel-Fatau Musah (kushoto), Mkuu wa Majeshi wa Nigeria Jenerali Christopher Musa (katikati) na Mkuu wa Majeshi wa Ghana Seth Amoama (kulia) wakijadiliana baada ya mkutano usio wa kawaida mjini Abuja, Nigeria, kuhusu machafuko ya kisiasa katika Jamhuri ya Niger, Agosti 2, 2023.
Kamishna wa Masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), Balozi Abdel-Fatau Musah (kushoto), Mkuu wa Majeshi wa Nigeria Jenerali Christopher Musa (katikati) na Mkuu wa Majeshi wa Ghana Seth Amoama (kulia) wakijadiliana baada ya mkutano usio wa kawaida mjini Abuja, Nigeria, kuhusu machafuko ya kisiasa katika Jamhuri ya Niger, Agosti 2, 2023. AFP - KOLA SULAIMON
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu unakuja saa chache baada ya mapendekezo ya Wakuu wa Nchi na Serikali za ECOWAS waliokusanyika katika Mkutano wa kilele huko Abuja, nchini Nigeria mnamo Agosti 11.

Wakuu wa majeshi ya nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) watakutana Agosti 12, 2023 mjini Accra, kufuatia ombi la kukitaka kikosi hiki kuwa kujiandaa na kupelekwa nchini Niger kurejesha utawala wa kikatiba, baada ya kushindwa kwa njia za kidiplomasia, kulingana na ripoti ya mwandishi wetu huko Cotonou, Jean-Luc Aplogan.

"Maagizo tuliyopewa yako wazi", anaeleza afisa mkuu wa jeshi la Afrika Magharibi: "kujiandaa na kutumwa nchini Niger bila kuchelewa", ameongeza afisa huyo mkuu wa jeshi kutoka moja ya nchi za Afrika Magharibi.

Mkutano huo utafanyika mjini Accra Jumamosi hii. Ghana ina historia ya kuandaa mikutano ya Wakuu wa majeshi kwa miradi ya operesheni ya pamoja. Mikutano kadhaa kuhusu Accra Initiative, jukwaa la usalama ambalo limekuwa likifanyika kila mwaka tangu 2017, iliandaliwa nchini humo.

Kulingana na hali inayotarajiwa, kikosi hiki kitaundwa na wanajeshi 25,000. Mbali na wanajeshi wa Côte d'Ivoire, kikosi hicho kitaundwa na wanajeshi kutoka Nigeria, Benin na Senegal. Sehemu kubwa ya askari watakuwa wa Nigeria.

Wakati wa Mkutano usio wa kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa ECOWAS, mnamo Agosti 10 huko Abuja, Guinea-Bissau pia ilithibitisha ushiriki wake. Cape Verde na Sierra Leone zimeonyesha kuunga mkono kikosi hicho, amesema mmoha wa washiriki wa mkutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.