Pata taarifa kuu

Niger yafunga anga kwa kuhofia 'uvamizi' kutoka kikosi cha ECOWAS

Licha ya kumalizika kwa makataa yaliyowekwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), serikali ya Niger haijaonyesha nia ya kumrejesha madarakani Rais Mohamed Bazoum. Jioni ya Jumapili Agosti 6, Baraza la Ulini wa Taifa (CNSP) lilichapisha taarifa kadhaa kwa vyombo vya habari ambazo zinaonyesha shinikizo linaloongezeka kwautawala wa kijeshi.

Picha hii ya skrini ya video kutoka ORTN - Télé Sahel mnamo Julai 31, 2023 inamuonyesha Kanali-Meja Amadou Abdramane akisoma taarifa kwenye televisheni ya taifa.
Picha hii ya skrini ya video kutoka ORTN - Télé Sahel mnamo Julai 31, 2023 inamuonyesha Kanali-Meja Amadou Abdramane akisoma taarifa kwenye televisheni ya taifa. © AFP -
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyosomwa Jumapili jioni, CNSP inaeleza kwamba ina taarifa zinazoonyesha kwamba "majeshi ya taifa la kigeni yanajiandaa kushambulia Niger na raia wake", bila kubainisha ni lipi.

Taarifa nyingine kwa vyombo vya habari inatangaza "kwamba kutumwa kabla ya vikosi vinavyopaswa kushiriki katika vita hivi kumeanza katika nchi mbili za Afrika ya Kati", tena bila kutaja majina ya nchi hizo. Lakini taarifa hiyo inaongeza kuwa "nchi yoyote ambayo hatua za kijeshi zitaelekezwa dhidi ya Niger itachukuliwa kuwa muasi".

Kulingana na CNSP, dalili ya kuongezeka kwa shinikizo na, "tishio la kuingilia kati ambalo linazidi kuwa wazi kutoka nchi jirani", Niger pia imefunga anga yake. Na taarifa kwa vyombo vya habari inaahidi kwamba "ukiukwaji wowote utakuwa somo la majibu ya nguvu na ya papo hapo".

Taarifa hiyo inamalizia kwa kuhakikisha kwamba "vikosi vya kijeshi vya Niger na vikosi vya ulinzi na usalama viko tayari kutetea uadilifu wa eneo letu na heshima ya nchi yetu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.