Pata taarifa kuu

Nigeria: Bunge la Seneti lapaza sauti dhidi ya operesheni ya kijeshi nchini Niger

Jumapili hii, Agosti 6 itakuwa siku ya mwisho ya makataa yaliyotolewa na ECOWAS kwa viongozi wa mapinduzi nchini Niger kuachia madaraka. Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi inatishia wanajeshi waliofanya mapinduzi kwa kuingilia kijeshi nchini Niger.  

Rais wa Nigeria Bola Tinubu alichaguliwa kuwa rais wa ECOWAS mnamo Julai 9, 2023 huko Bissau.
Rais wa Nigeria Bola Tinubu alichaguliwa kuwa rais wa ECOWAS mnamo Julai 9, 2023 huko Bissau. REUTERS - TEMILADE ADELAJA
Matangazo ya kibiashara

Nigeria, nchi kubwa ya kikanda, inaweza kuchukua jukumu kuu katika operesheni hii. Nchi hiyo pia inashikilia uenyekiti wa Cédéo. Lakini nchini humo shinikizo la kisiasa ni kubwa kwa mkuu wa nchi, Bola Tinubu. Seneti pia imemtaka kupendelea chaguzi zingine.

Bola Tinubu aliwaandikia maseneta kuwataka waidhinishe maazimio ya ECOWAS. Lakini maseneta hawa hawakukukualiana na hoja hii ya mkuu wa nchi. Badala yake, baada ya saa kadhaa za kikao chao, maseta hatimaye waamemwomba rais Bola Tinubu kuimarisha chaguzi za kidiplomasia na kisiasa kutatua mgogoro nchini Niger.

Katika majibu yake, Bunge la Seneti lilitupilia mbali mapinduzi ya kijeshi, lakini pia linaonyesha kusita kwake dhidi ya makabiliano ya kijeshi.

Tayari Ijumaa jioni, maseneta wa Kaskazini, wao, walikuwa na wasiwasi kuhusu athari za operesheni ya kijeshi. Nchi hizo mbili zinashiriki kilomita 1,500 za mpaka na wawakilishi waliochaguliwa wa eneo hilo walikuwa wamesisitiza uhusiano wa kitamaduni, kidini na lugha kati ya pande hizo mbili. Kwa hiyo walionya dhidi ya "matumizi ya nguvu kabla ya kumaliza njia zote za kidiplomasia", na kuongeza kuwa operesheni itakuwa na "madhara nchini Nigeria" na uwezekano wa kuvuruga kwa maeneo maskini sana ambayo tayari yameshinikizwa na makundi yenye silaha.

Hatimaye, shinikizo la kisiasa limeongezeka zaidi kwa Bola Tinubu kwa maneno makali ya CUPP. Siku ya Jumamosi asubuhi, muungano mkubwa zaidi wa upinzani ulmeshutumu mpango wa kijeshi "sio tu usio na maana, lakini kutowajibika". "Nigeria haiwezi kumudu kupoteza rasilimali zake zinazopungua na maisha ya thamani ya wanajeshi wetu. Mtazamo mpya unaweza kutumbukiza uchumi dhaifu katika mgogoro mkubwa zaidi, "wapinzani wamesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.