Pata taarifa kuu

Mmoja wa majenerali walioongoza mapinduzi Niger amewasili jijini Bamako

Nairobi – Jenerali Salifou Mody, mmoja wa wanajeshi walioongoza mapinduzi ya kijeshi nchini Niger wiki iliyopita, amewasili katika nchi jirani ya Mali ambako kiongozi wake wa kijeshi ameunga mkono mapinduzi hayo wakati huu Niger ikiendelea kukabiliwa na shinikizo la kimataifa.

Licha ya kuthibitisha kuwasili kwa ujumbe huo, sababu kuu ya ziara hiyo haikuwekwa wazi.
Licha ya kuthibitisha kuwasili kwa ujumbe huo, sababu kuu ya ziara hiyo haikuwekwa wazi. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mody, mkuu wa zamani wa jeshi ambaye alitimuliwa katika nafasi hiyo mwezi Aprili, aliwasili jijini Bamako kabala ya ujumbe mwengine kutoka Niamey, imethibitisha taarifa ya afisa wa ngazi ya juu nchini Niger na ofisa wa usalama kutoka upande wa Bamako.

Licha ya kuthibitisha kuwasili kwa ujumbe huo, sababu kuu ya ziara hiyo haikuwekwa wazi.

Jeshi nchini limekuwa linakabiliwa na shinikizo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa wakati Ecowas nayo ikitishia kutumia nguvu iwapo rais Mohamed Bazoum hatarejeshwa madarakani.

Haya yanajiri wakati huu ambapo mawaziri wa usalama kutoka mataifa ya Ecowas wakikutana mjini Abuja nchini Nigeria kujadili mapinduzi ya kijeshi yaliotokea nchini Niger wiki iliyopita.

Kando na hayo, ujumbe mwengine ukiongozwa na rais wa zamani wa Nigeria Abdulsalami Abubakar ukitarajiwa nchini Niger.

Tayari uongozi wa kijeshi nchini Mali na Burkina Faso, ambao pia ulioongoza mapinduzi kati ya mwaka wa 2020 na 2022 umeonya kujibu iwapo mataifa mengine yataingilia kinachoendelea Niger.

Nchi zote za Sahel zinakabiliwa na changamoto za kiusalama, makundi ya watu wenye silaha yakionekana kutawala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.