Pata taarifa kuu

Hali ya wasiwasi yatanda nchini Niger, baada ya kumalizika kwa makataa ya ECOWAS

Nchini Niger, muda wa makataa uliotolewa na ECOWAS umekwisha. Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ilitoa hadi Jumapili, Agosti 6 saa sita usiku huko Niamey kwa wanajeshi waliompindua Rais Mohamed Bazoum kurejesha utulivu wa kikatiba. Muda wa makataa tayari umemalizika yapata, wakati ECOWAS ilikuwa imetaja uwezekano wa kuingilia kijeshi ikiwa waasi watang'ang'ania mamlakani. Sasa hali ya wasi wasi imetanda nchini Niger.

Wakuu wa majeshi kutoka nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), isipokuwa Mali, Burkina Faso, Chad, Guinea na Niger, wakipiga picha ya pamoja wakati wa mkutano wao usio wa kawaida mjini Abuja, Nigeria, Ijumaa, Agosti 4, 2023, kujadili hali nchini Niger.
Wakuu wa majeshi kutoka nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), isipokuwa Mali, Burkina Faso, Chad, Guinea na Niger, wakipiga picha ya pamoja wakati wa mkutano wao usio wa kawaida mjini Abuja, Nigeria, Ijumaa, Agosti 4, 2023, kujadili hali nchini Niger. AP - Chinedu Asadu
Matangazo ya kibiashara

Muda umeisha na wanajshi bado wanashikilia mamlaka. Hali hiyo sasa inahitaji maswali mengi lakini majibu machache. ECOWAS ilizungumzia kuhusu "operesheni ya kijeshi inayowezekana" na wakuu wake majeshi kutoka jumuiya hiyo walitangaza uwezekano wa kuingilia kijeshi nchini Niger kwa muda wowote baada ya kumalizika kwa makataa ya ECOWAS. Vyanzo vingine vilisema kwamba jeshi la ECOWAS liko tayari.

Lakini haiwezekani kujua kama ECOWAS itachukua mkondo huo, wakati wanajeshi wa Niger walikuwa wameahidi kujihami ikiwa watashambuliwa. Pia ni vigumu kuamua kwa sasa kama kulikuwa na sehemu ya makubaliano katika maazimio ya kambi hizo mbili.

Kwa vyovyote vile, shinikizo ni kubwa kwa ECOWAS. Mali na Burkina Faso, ambazo zinaoongozwa na wanajshi, zilitangaza hivi karibuni kwamba zinatalichukulia shambulio lolote dhidi ya Niamey kama tangazo la vita. Mataifa yasiyo wanachama lakini yenye ushawishi mkubwa, kama vile Chad na Algeria, yametangaza kwamba yanapinga kabisa uingiliaji kati kwa kutumia silaha.

Shinikizo pia kwa Bola Tinubu. rais wa ECOWAS na mkuu wa nchi wa Nigeria ameiweka nchi yake katika mstari wa mbele, huku sauti kadhaa zikitolewa nchini Nigeria kuzuia kuzuka kwa mapigano. Nchini Niger, hali ya wasiwasi imetanda, huku maelfu ya watu walikusanyika siku ya Jumapili katika uwanja wa Niamey kuwaunga mkono wanajeshi wanaoshikilia mamlaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.