Pata taarifa kuu

Niger: Jenerali Tchiani, mkuu mapinduzi, afanya uteuzi mpya ndani ya jeshi

Kiongozi mkuu wa mapinduzi nchini Niger, Jenerali Abdourahame Tchiani, alifanya uteuzi mpya ndani ya jeshi siku ya Ijumaa Agosti 4. Takriban wakuu wote wa majeshi ambao hata hivyo walijiunga na wanajeshi waliofanya mapinduzi wamebadilishwa. Maafisa walio husiano wa karbu na washirika wamepandishwa vyeo.

Jenerali Abdourahamane Tchiani wakati wa hotuba yake kwenye Télé Sahel, Julai 28, 2023.
Jenerali Abdourahamane Tchiani wakati wa hotuba yake kwenye Télé Sahel, Julai 28, 2023. © RTN
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel

Mkuu mpya wa majeshi ya Niger ni Jenerali Moussa Salaou Barmou. Hadi wakati huu, amekuwa akiongoza Kikosi Maalum cha Niger, katika mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Jenerali Barmou amefuata kozi kadhaa za mafunzo nchini Marekani. Alikuwa mshirika mkubwa wa kiongozi wa mapinduzi wakati wa mapinduzi ya mwisho huko Niamey. Naibu wake ni Kanali-Meja Amirou Abdoul Kader. Uteuzi wake unaashiria mwisho wa sintofahmu ambayo itakuwa imechukua miezi kadhaa. Katika uongozi wa jeshi la nchi kavy, ameteuliwa afisa mwingine, kutoka kikosi maalum kinachosimamia mapambano dhidi ya ugaidi.

Kwa kufanya mabadiliko haya kwenye uongozi wa FDS, Jenerali Abdourahame Tchiani, kwanza anataka kuonyesha kwamba anadhibiti jeshi , lakini zaidi ya yote kuunganisha ushirikiano ndani ya majeshi. Pia pengine alitaka kutegemea wanajeshi waaminifu. Kwa kudhihirisha dhamira hiyo, amemteuwa Kamanda Mkuu mpya wa kikosi cha askari jeshi, Kanali-Meja Karim Hima, mwanafunzi mwenzake katika shule ya kijeshi huko Thiès, nchini Senegal.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.