Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-USALAMA

Niger: Maadhimisho ya uhuru yagubikwa na maandamano ya kuunga mkono viongozi wa mapinduzi

Tarehe 3 Agosti Niger inaadhimisha miaka 63 ya uhuru wake. Lakini mwaka huu, hakuna gwaride la kijeshi. Asubuhi hii, maandamano yalifanyika Niamey, ambapo mamia ya waandamanaji walianadaman kuunga mkono wanajeshi.

Wafuasi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Niger wakikusanyika kwa maandamano yaliyoitishwa kupigania uhuru wa nchi hiyo na kuzuia kuingiliwa na mataifa ya kigeni, huko Niamey, Niger, Alhamisi, Agosti 3, 2023.
Wafuasi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Niger wakikusanyika kwa maandamano yaliyoitishwa kupigania uhuru wa nchi hiyo na kuzuia kuingiliwa na mataifa ya kigeni, huko Niamey, Niger, Alhamisi, Agosti 3, 2023. © Sam Mednick / AP
Matangazo ya kibiashara

Huko Niamey, maandamano yalikamilika mchana, Agosti 3, 2023. Mkutano wa hadhara umeratibiwa kufanyika Alhamisi saa tisa alaasiri, katika uwanja wa General Seyni Kountché.

Asubuhi ya leo, maelfu ya watu, hasa wanaume na vijana, walikusanyika kwenye eneo la Place de la Concertation kwa mkutano wa saa mbili ambapo hotuba kadhaa zilitolewa, hasa na viongozi na wawakilishi wa mashirika ya kiraia, kutoka muungano wa M62, unaojulikana kwa misimamo yake dhidi ya uwepo wa jeshi la Ufaransanchini Niger.

Katika mkutano huo watu wengi walionekana wakivalia nguo zenye picha ya Jenerali Abdourahmane Tiani, kamanda wa kikosi cha walinzi wa rais, mmoja wa viongozi wa mapinduzi na rais wa utawala wa kijeshi kutoka Kamati ya Ulinzi wa Taifa (CNSP) na wakibebelea bendera kadhaa za Urusi.

Maneno dhidi ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) pia yalisikika. ECOWAS ilitoa makataa ya wiki moja kwa viongozi wa mapinduzi kuweka chini silaha zao. Maneno mengine pia yalisikika dhidi ya uwepo wa jeshi la Ufaransa nchini Niger. Waandamanaji waliandamana kwa amani mbele ya Ubalozi wa Ufaransa, bila makabiliano.

Wanajeshi kutoka kikoi cha walinzi wa taifa cha Niger walitenga eneo salama kati ya balozi ya Ufaransa na waandamanaji.

Katika mkoa wa Agadez, huko pia mamia ya watu walijitokeza kuunga mkono wanajeshi. Hii ni mara ya kwanza katika jiji hili muhimu, linalopatikana katikati mwa nchi ambalo lilikuwa bado halijaonesha upande wowote linaloegemea tangu kuanza kwa mzozo huo.

Hali ni shwari kwa sasa huko Maradi, mji mkuu wa kiuchumi ulioko kilomita kadhaa kutoka mpaka na Nigeria. Mji huu unakabiliwa na mzigo mkubwa wa vikwazo vya ECOWAS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.