Pata taarifa kuu

Niger: Mapinduzi yanaweza kuwa na athari kwa ulimwengu, aonya rais Mohamed Bazoum

Akiwa bado anazuiliwa na wanajeshi waliofanya mapinduzi katika makazi yake, rais wa Niger Mohamed Bazoum, aliyepinduliwa Julai 26, amezungumza katika safu iliyochapishwa katika Gazeti la kila siku la Marekani la Washington Post Alhamisi jioni Agosti 3.Β 

Rais wa Niger Mohamed Bazoum (picha ya zamani), hapa ilikuwa wakati wa mkutano na Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Ufaransa wakati wa ziara yao huko Niamey, Julai 15, 2022.
Rais wa Niger Mohamed Bazoum (picha ya zamani), hapa ilikuwa wakati wa mkutano na Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Ufaransa wakati wa ziara yao huko Niamey, Julai 15, 2022. Β© Bertrand Guay / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Mohamed Bazoum anabaini kwamba mapinduzi ya Niger yanaweza kuwa na athari kubwa kwa ulimwengu na kuleta kanda nzima ya Sahel chini ya "ushawishi" wa Urusi, kupitia mamluki wa kundi la Wagner.Β 

"Ninatoa wito kwa serikali ya Marekani na jumuiya nzima ya kimataifa kusaidia kurejesha utaratibu wa kikatiba," ameongeza.

Hayo yanajiri wakati wanajeshi wanaoshikilia madaraka nchini Niger wameonya kuwa "uchokozi au jaribio lolote la uvamizi wa ECOWAS litakabiliwa na jibu kali kutoka vkosi vya Ulinzi na usalama vya Niger.

Hayo ni baada ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi kutoka makataa hadi Jumapili Agosti 6 wanajeshi wanaoshikilia mamlaka nchini Niger wawe wamerejesha utaratibu wa kikatiba na kumkabidhi madaraka rais aliyetimuliwa mamlakani Mohamed Bazoum.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.