Pata taarifa kuu

Niger yafungua mipaka yake ya ardhini na angani na nchi tano jirani

Mipaka ya ardhini na angani ya Niger na nchi tano jirani imefunguliwa tena, karibu wiki moja baada ya kufungwa kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomtimua mamlakani rais mteule Mohamed Bazoum, mmoja wa viongozi wa mapinduzi alitangaza kwenye televisheni siku ya Jumanne usiku.

Ndege ya kwanza ya Ufaransa iliyokuwa imebeba watu 262 waliohamishwa kutoka Niger ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Paris-Roissy Charles de Gaulle muda mfupi baada ya saa saba na nusu usiku wa Jumanne Agosti 1 kuamkia Jumatano Agosti 2, chanzo kwenye uwanja wa ndege kimeliambia shirika la habari la AFP, siku chache baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini humo.2023.
Ndege ya kwanza ya Ufaransa iliyokuwa imebeba watu 262 waliohamishwa kutoka Niger ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Paris-Roissy Charles de Gaulle muda mfupi baada ya saa saba na nusu usiku wa Jumanne Agosti 1 kuamkia Jumatano Agosti 2, chanzo kwenye uwanja wa ndege kimeliambia shirika la habari la AFP, siku chache baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini humo.2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Mipaka ya ardhini na angani imefunguliwa kwa nchi za Algeria, Burkina Faso, Libya, Mali na Chad"  "kuanzia leo", ametangaza, saa chache baada ya Ufaransa kuondoa kundi la kwanza la wa raia wake na siku tano kabla ya kumalizika kwa muda uliotolewa ECOWAS kurejesha utaratibu wa kikatiba.

Ndege ya kwanza ya Ufaransa iliyokuwa imebeba watu 262 waliohamishwa kutoka Niger ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Paris-Roissy Charles de Gaulle muda mfupi baada ya saa saba na nusu usiku wa Jumanne Agosti 1 kuamkia Jumatano Agosti 2, chanzo kwenye uwanja wa ndege kimeliambia shirika la habari la AFP, siku chache baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini humo.

"Kuna watu 262 kwenye ndege hiyo, ambayo ni Airbus A330, ikiwa ni pamoja na watoto kumi na wawili," Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Catherine Colonna aliliambia shirika la habari la AFP Jumanne jioni , akieleza kuwa "takriban abiria wote ni raia wa Ufaransa".

Mbali na idadi kubwa ya Wafaransa, pia walikuemo Waniger, Wareno, Wabelgiji, Waethiopia na Walebanon, Wizara ya Mambo ya Nje iliwaambia waandishi wa habari waliokuwepo kwenye uwanja wa ndege wa Roissy.

Ndege ya pili inatarajia kutua kwenye uwanja huo, ikiwa na Wafaransa, Wanigeria, Wajerumani, Wabelgiji, Wacanada, Wamarekani, Waaustria na Wahindi, kulingana na chanzo kimoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.