Pata taarifa kuu

Mataifa ya kigeni yaanza kuwaondoa raia wake Niger kufuatia mapinduzi

NAIROBI – Nchi ya Ufaransa, Italia pamoja na mataifa mengine ya Ulaya, hivi leo yameanza mchakato wa kuwaondoa raia wake walioko Niger.

Wanajeshi wa Ufaransa wakiwasaidia raia kuingia kwenye basi kabla ya kusafirishwa kwa ndege hadi Ufaransa, katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Niamey, Niger, Jumanne, Agosti 1, 2023.
Wanajeshi wa Ufaransa wakiwasaidia raia kuingia kwenye basi kabla ya kusafirishwa kwa ndege hadi Ufaransa, katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Niamey, Niger, Jumanne, Agosti 1, 2023. AP - Sam Mednick
Matangazo ya kibiashara

Ni siku 6 sasa tangu wanajeshi wapindue serikali ya rais Mohamed Bazoum, anayeungwa mkono na nchi za magharibi katika vita dhidi ya makundi ya kijihadi.

Hatua ya Ufaransa imekuja baada ya siku ya Jumapili, waandamanaji wanaoliunga mkono Jeshi, kuvamia ubalozi wake mjini Niamey, ambapo ilionya itachukua hatua ikiwa raia na maslahi yake yatalengwa.

Kwa mujibu wa takwimu za mataifa haya, Ufaransa, Italia, Ujerumani na mataifa mengine, yana zaidi ya raia elfu moja kuanzia mjini Niamey na maeneo mengine ya taifa hilo.

Aidha mataifa haya licha ya kutokuwa na idadi kamili ya raia wake walioko Niger, pia hayajasema ni raia wangapi ambao wamekataa kuondoka, kama anavyoeleza kanali Michael Goya, mtaalamu wa masuala ya kijeshi.

Raia wa kigeni kawaida wanajulikana na wamesajiliwa, wanaweza kutafutwa kwa urahisi. Kwa hivyo wakati wa kuwaondoa kila mtu anapewa taarifa ya kukutana sehemu moja kwa mfano uwanja wa ndege na kama wako mbali sana tutawafuata nyumbani kwa kutumia magari ya kijeshi.

00:18

Kanali Michel Goya, mtaalamu wa masuala ya kijeshi 1.08.23

Vyanzo kutoka wizara ya ulinzi ya Ufaransa, vinasema Paris itatuma ndege nne za kijeshi zenye uwezo wa kubeba watu 200 na tayari moja ilisharuka kuelekea Niamey, Kanali Goya hata hivyo akisema kuna uwezakano wa zoezi lisifanikiwe asilimia 100.

 

Hatari ni ikiwa tu hali itabadilika sana kwenye mji mkuu, haswa kama kuna maandamano dhidi ya Ufaransa au tishio baya zaidi lakini kwa sasa hakuna hiyo hatari. Ameongeza kanali Goya.

00:10

Kanali Michel Goya 2 01.08

Licha ya utawala wa kijeshi wa Niger kuruhusu mataifa hayo kutumia anga yake, kumekuwa na hofu kuwa huenda kukafanyika hujuma kufanya zoezi hilo lisifanyike kwa ufanisi, kutokana na mvutano ambao tayari umejitokeza kati yake na nchi za Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.