Pata taarifa kuu
AJALI-USALAMA

Ajali ya basi kaskazini mwa Senegal yaua ishirini na tatu

Watu 23 walifariki katika ajali ya basi iliyotokea Jumatano asubuhi kaskazini mwa Senegal, Rais Macky Sall ametangaza.

Mkasa huo ulitokea wakati basi lililokuwa limebeba abiria lilipopinduka katika kijiji cha Ngeune Sarr, eneo la Louga (picha ya zamani).
Mkasa huo ulitokea wakati basi lililokuwa limebeba abiria lilipopinduka katika kijiji cha Ngeune Sarr, eneo la Louga (picha ya zamani). © Cheikh Dieng / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Bado natoa wito kwa tahadhari zaidi barabarani," Rais Sall amesema katika ujumbe uliotumwa kwenye Twitter, iliopewa jina la "X".

Ripoti ya awali iliyowasilishwa kwa shirika la habari la AFP na afisa wa kikosi cha Zima moto ilisema watu 22 walifariki na 52 kujeruhiwa katika ajali hii. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya eneo hilo, mtu mmoja aliyejeruhiwa alifariki dunia, na kufanya idadi ya waliofariki kufikia 23.

Mkasa huo ulitokea wakati basi lililokuwa limebeba abiria lilipopinduka katika kijiji cha Ngeune Sarr, katika eneo la Louga, kulingana na kikosi cha Zima moto.

Mazingira ya ajali hayakutajwa na kikosi cha Zima moto. Waziri wa Mambo ya Ndani Antoine Félix Abdoulaye Diome alitembelea eneo la ajali siku ya Jumatano, kulingana na shirika la habari la AFP, likinukuu mjumbe wa msafara wa waziri. Watu 19 walifariki na 24 kujeruhiwa mnamo Januari 16 baada ya basi kugongana na lori katika eneo lililo karibu na Louga ambapo ajali ya Jumatano ilitokea.

Hapo awali, ajali nyingine ya mabasi mawili kugongana ilisababisha vifo vya karibu watu 40 mnamo Januari 8 katikati mwa nchi. Mkasa huo wa Januari 8, uliotokana na kupasuka kwa tairi, uliibua wimbi la shutuma dhidi ya mamlaka kwa kushindwa kusimamia sheria za maadili, lakini pia kanuni za hali ya magari, licha ya kuongezeka kwa ajali.

Serikali ya Senegal ilitangaza mara moja baadhi ya hatua ishirini, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku safari za usiku kwa mabasi na matairi yaliyotumiwa. Lakini nyingi ya hatua hizi zilikataliwa kuwa hazitumiki na wataalamu wa masuala ya uchukuzi.

Ajali hizi mwanzoni mwa mwaka zilidhihirisha ubovu wa barabara nchini Senegal, kama ilivyo katika nchi nyingi za Kiafrika: mpangilio mbaya na hatari wa magari, kuendesha gari kwa uzembe, au hata ufisadi ulioenea wa maafisa wanaowajibika kutekeleza sheria au utoaji wa leseni ya udereva.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.