Pata taarifa kuu
USALAMA BARABARANI

Senegal: Zaidi ya watu 38 wafariki na 87 kujeruhiwa baada ya mabasi mawili kugongana

Watu zaidi ya 38 wamefariki dunia na 87 kujeruhiwa baada ya mabasi mawili kugongana usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili karibu na mji wa Kaffrine, kilomita 250 kusini Mashariki mwa mji mkuu wa Senegal, Dakar kulingana na taarifa kutoka polisi.

Ajali ya barabarani kufuatia kugongana kwa mabasi mawili, Januari 8, 2023, katika eneo la Sikio, katika mji wa Kaffrine, nchini Senegal.
Ajali ya barabarani kufuatia kugongana kwa mabasi mawili, Januari 8, 2023, katika eneo la Sikio, katika mji wa Kaffrine, nchini Senegal. AFP - CHEIKH DIENG
Matangazo ya kibiashara

 

Hii ndiyo ajali mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni kwa nchi hii ya Afrika Magharibi. Rais Macky Sall ametangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu.

Matengenezo duni ya magari na miundombinu ya barabara

Waathiriwa wamesafirishwa hospitalini huko Kaffrine, mabaki ya mabasi yameondolewa na barabara imefunguliwa tena, kulingana na kikosi cha Zima moto. Mkuu wa mkoa na maafisa kadhaa wa mji huo wamekwenda katika eneo la tukio.

Ajali za mabasi ni za hutokea mara nyingi barani Afrika, kutokana na matengenezo duni ya magari, ubovu wa barabara na makosa ya madereva. Madereva wengi wana leseni zilizonunuliwa kutoka kwa wakaguzi wafisadi, bila hata hivyo kuhudhuria shule ya udereva.

Katika bara la Afrika, aina hii ya ajali imeongezeka. Wiki iliyopita, takriban watu kumi na wanne walifariki dunia nchini Côte d'Ivoire na 73 kujeruhiwa katika baada ya mabasi mawili kugongana uso kwa uso huko Yamoussoukro, katikati mwa nchi, na watu 18 walifariki dunia baada ya magari mawili kugongana kaskazini mwa Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.