Pata taarifa kuu

Niger: Watatu wamefariki katika ajali ya helikopta ya kijeshi

Watu watatu wamefariki Jumatatu katika ajali ya helikopta ya kijeshi kwenye kambi ya jeshi la Niger, karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Niamey, imebaini wizara ya Ulinzi.

Mwanajeshi wa Niger akitoa ulinzi kwenye barabara karibu na soko huko Banibangou, mji ulioko magharibi mwa Niger, mnamo Novemba 6, 2021, ambapo watu 69 walikufa katika shambulio la wanajihadi mnamo Novemba 2, 2021.
Mwanajeshi wa Niger akitoa ulinzi kwenye barabara karibu na soko huko Banibangou, mji ulioko magharibi mwa Niger, mnamo Novemba 6, 2021, ambapo watu 69 walikufa katika shambulio la wanajihadi mnamo Novemba 2, 2021. AFP - BOUREIMA HAMA
Matangazo ya kibiashara

"Jumatatu hii, Desemba 26, 2022 mwendo wa saa 4:40 asubuhi. kwa saa za huko, helikopta ya jeshi la Niger MI-17, ilipokuwa ikirejea kutoka kwenye safari ya kawaida ya mafunzo, ilianguka wakati ikitua kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi kutoka uwanja wa ndege wa Niamey," Wizara ya Ulinzi ya Nigeria imesema katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habarila AFP.

"Kwa bahati mbaya wafanyakazi watatu, mafisa wawili wa jeshi wa Niger na mkufunzi kutoka nchi ya kigeni walikufa papo hapo licha ya juhudi za idara huduma za dharura kudhibiti moto", imeongeza wizara hiyo.

Tume ya uchunguzi "iliundwa mara moja ili kujua sababu za ajali hii mbaya", taarifa ya Wizara ya Ulinzi imebainisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.