Pata taarifa kuu
USALAMA WA BARABARANI

Marufuku ya kusafiri usiku nchini Senegal

Serikali ya Senegal Iimetangaza leo Jumanne hatua mpya za kukabiliana na usalama barabarani, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku usafiri wa basi usiku na uingizaji wa matairi yaliyotumika, baada ya ajali iliyoua watu 39 siku ya Jumapili.

Mabasi mawili yaligongana na kusababisha vifo vya watu 39, siku ya Jumapili Januari 8, 2023, katika eneo la Sikio, katika jimbo la Kaffrine, nchini Senegal.
Mabasi mawili yaligongana na kusababisha vifo vya watu 39, siku ya Jumapili Januari 8, 2023, katika eneo la Sikio, katika jimbo la Kaffrine, nchini Senegal. AFP - CHEIKH DIENG
Matangazo ya kibiashara

Magari ya uchukuzi wa abiria yatapigwa marufuku "kusafiri kwenye barabara za mijini kati ya 5:00 usiku. na 11:00 alfajiri," Waziri Mkuu Amadou Bâ ametangaza baada ya mkutano wa serikali katika mji mpya wa Diamniadio, karibu na Dakar.

Mabasi yanayoitwa "ratiba", yanayosafirisha abiria na mizigo, ambayo mengi husafiri usiku kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine, ni moja ya njia kuu za usafiri nchini Senegal na husababisha ajali nyingi.

Hatua nyingine ni marufuku ya uingizaji wa matairi ya mitumba kutoka nje ya nchi na kufanya "lazima mabasi kuwa na mitambo inayohesabu mwendo kasi ya magari yanayosafirisha watu na mizigo kwa kasi ya kilomita 90 kwa saa" pia zimetangazwa katika mkutano wa Jumanne.

Maagizo yatatolewa ndani ya saa 72 ili kutekeleza hatua 23 mpya zilizotangazwa. Hatutakubaliana na wale wanaokiuka sheria zilizowekwa ili kuhakikisha usalama wa raia wenzetu," amesema Waziri Mkuu.

Ajali za barabarani huua rasmi watu 700 kila mwaka nchini Senegal, nchi ya Afrika Magharibi yenye zaidi ya wakaaji milioni 17.

Hatua hizo mpya zimetangazwa baada ya ajali ya mabasi mawili ambayo ilisababisha vifo vya watu 39 na kujeruhi 101 siku ya Jumapili katika kijiji cha Sikilo, jimbo la Kaffrine, katikati mwa n,chi, kilomita 250 kutoka Dakar. Rais Macky Sall, ambaye alizuru siku hiyo eneo la ajali, alitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.