Pata taarifa kuu

Watu 19 wafariki baada ya basi kugongana na lori nchini Senegal

Ajali ya basi kugongana uso kwa uso na lori ilisababisha vifo vya watu 19 nchini Senegal siku ya Jumatatu, wakati mamlaka ilipokabiliana na upinzani kutoka kwa magari ya uchukuzi dhidi ya hatua mpya zilizochukuliwa baada ya ajali nyingine mbaya wiki moja iliyopita.

Mnamo Januari 8, zaidi ya watu 40 waliuawa katika ajali ya mabasi mawili katikati ya nchi, na hivyo kubainisha shida za barabarani nchini Senegal kama ilivyo katika nchi nyingi za Kiafrika: uchakavu na mpangilio hatari wa magari, kuendesha kwa uzembe, au ufisadi mkubwa kwa maafisa wa polisi ya barabarani au kwa maafisa wa wanaoheshimosha sheria au kutoa leseni.
Mnamo Januari 8, zaidi ya watu 40 waliuawa katika ajali ya mabasi mawili katikati ya nchi, na hivyo kubainisha shida za barabarani nchini Senegal kama ilivyo katika nchi nyingi za Kiafrika: uchakavu na mpangilio hatari wa magari, kuendesha kwa uzembe, au ufisadi mkubwa kwa maafisa wa polisi ya barabarani au kwa maafisa wa wanaoheshimosha sheria au kutoa leseni. AFP - CHEIKH DIENG
Matangazo ya kibiashara

"Kumetokea ajali nyingine mbaya katika moja ya barabara zetu kwenye lango la Ngeun Sarr. Watu 19 wamepoteza maisha", ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Rais wa Senegal Macky Sall. Ajali hii ilitokea karibu na mji wa Louga, kaskazini mwa nchi, pia umesababisha watu 25 kujeruhiwa, Kanali Papa Ange Michel Diatta, afisa wa idara ya Zima moto, ameliambia shirika la habari la AFP.

Mnamo Januari 8, zaidi ya watu 40 waliuawa katika ajali ya mabasi mawili katikati ya nchi, na hivyo kubainisha shida za barabarani nchini Senegal kama ilivyo katika nchi nyingi za Kiafrika: uchakavu na mpangilio hatari wa magari, kuendesha kwa uzembe, au ufisadi mkubwa kwa maafisa wa polisi ya barabarani au kwa maafisa wa wanaoheshimosha sheria au kutoa leseni.

Shahidi aliyehojiwa na redio binafsi ya RFM aliripoti kuwa siku ya Jumatatu asubuhi basi hilo liliyumba baada ya kujaribu kumkwepa punda, maelezo ambayo hayajathibitishwa kwingine. Mifugo ni wengi kutangatanga au kuwa kando ya barabara nchini Senegal.

Mkasa huo wa Januari 8, uliotokana na kupasuka kwa tairi, ulizua ulisababisha ukosoaji mkubwa dhidi ya viongozi kwa kushindwa kusimamia sheria za maadili, lakini pia kanuni za masharti ya magari.

Serikali ilitangaza zaidi ya hatua ishirini, kufuatia ajali hii, mojawapo ya ajali mbaya zaidi nchini Senegal katika miaka ya hivi karibuni.

Ajali hiyo ya kaskazini "inaangazia haja ya kuimarisha hatua za usalama barabarani", alisema rais wa Senegal.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.