Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Ukraine na Urusi kila moja alaani shinikizo kwa mataifa ya Afrika

Katika mkesha wa mkutano wa kilele wa Urusi na Afrika, utakaofanyika Alhamisi Julai 27 na Ijumaa Julai 28 huko St. Petersburg, diplomasia ya Ukraine na Urusi zinajaribu kuwahamasisha washirika wao katika bara hilo. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kouleba (kushoto) na msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov (kulia).
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kouleba (kushoto) na msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov (kulia). © Mary Altaffer & Valery Sharifulin (Sputnik), AP - Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kouleba akilaani mkutano wa kilele unaolenga kurejesha sura ya Vladimir Putin, msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov badala yake anazituhumu nchi za Magharibi kwa kuweka shinikizo kwa viongozi wa Afrika.

Dmitri Peskov anasema, hakuna shaka kwamba nchi za Magharibi zimefanya kila linalowezekana kuhujumu mkutano wa kilele wa Urusia na Afrika. "Takriban mataifa yote ya Afrika yamekabiliwa na shinikizo ambalo halijawahi kutokea kutoka Marekani. Misheni nyingine za Magharibi pia zinajaribu kushiriki katika juhudi hizi za kuzuia mkutano huu usifanyike, ili kuzuia mataifa haya ya Afrika kuwakilishwa katika mkutano huu,” amesema.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kouleba ameongeza safari zake barani Afrika katika miezi ya hivi karibuni. Kutoka Malabo, nchini Equatorial Guinea alikokuwa siku ya Jumanne Julai 25, hata hivyo alihakikisha kwamba ataheshimu uamuzi huru wa nchi zilizoalikwa za Afrika. Hata hivyo, anazionya kuhusu nia ya Urusi: “Tunaheshimu uamuzi unaochukuliwa na kila nchi kwa kuzingatia maslahi yake ya kitaifa. Lakini ninachojaribu kuwaeleza wenzangu wa Afrika ni kwamba Rais Putin atatumia mkutano huu kujaribu kujisafisha. Lengo ni kufanya propaganda. "

Naye rais wa Urusi anasema mkutano huu utakuwa fursa ya kuonyesha uelewa wake na washirika wake wa Afrika, licha ya mzozo wa Ukraine na kutamatika kwa makubaliano ya nafaka, ikiwa ni chanzo cha wasiwasi katika bara la Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.