Pata taarifa kuu

Algeria: Takriban watu 34 wafariki wakiwemo wanajeshi 10 katika mkasa wa moto mkali

Takriban watu 34, wakiwemo wanajeshi kumi, wamefariki katika mkasa wa moto mkali uliotokea kaskazini mashariki mwa Algeria usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu na bado moto huo unaendelea, kulingana na ripoti iliyochapishwa na Wizara ya Mambo ya Ndani Jumatatu usiku.

Moto waripotiwa katika eneo la Melloula kaskazini magharibi mwa Tunisia, karibu na mpaka na Algeria, mnamo Julai 24, 2023.
Moto waripotiwa katika eneo la Melloula kaskazini magharibi mwa Tunisia, karibu na mpaka na Algeria, mnamo Julai 24, 2023. Β© FETHI BELAID / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi walijikuta wakizingirwa na miali ya moto walipokuwa wakihamishwa kutoka Beni Ksila, katika wilaya ya mashariki ya BΓ©jaΓ―a, wakiandamana na wakazi wa vijiji jirani, Wizara ya Ulinzi imesema. Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune ametuma salamu za rambirambi kwa familia, akitaja kuwa miongoni mwa wahanga kuna 'kiraia' lakini pia 'wanajeshi'.

Katika nchi jirani ya Tunisia, katika eneo la mpaka la Tabarka kaskazini-magharibi, mikasa ya moto mkali ulianza tena Jumatatu karibu na eneo ambalo tayari limeharibiwa na moto wiki iliyopita. Kulingana na shirika la habari la AFP, timu ya wanahabari wake waliweza kuona uharibifu mkubwa karibu na eneo la Nefza, kilomita 150 magharibi mwa Tunis, ambapo helikopta na ndege maalumu katika shughuli ya uokoaji za Canadair ziliingilia kati kwa kujaribu kuzima moto huo.

"Wakazi wapatao 300 wa kijiji cha Melloula walihamishwa kwa njia ya bahari" kama tahadhari dhidi ya dhoruba kali za upepo zinazochochea moto huo, kulingana na Houcem Eddine Jebabli, msemaji wa kikosi cha walinzi wa kitaifa nchini Tunisia, ambaye pia amebaini kwamba watu kadhaa wameondoka makaazi yao kwa kutumia njia ya nchi kavu. "Walihamishiwa kwenye vituo vya mapokezi huko Tabarka au kupewa hifadhi na ndugu zao," Moez Triaa, msemaji wa kikosi cha walinzi wa raia, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kati ya Jumapili na Jumatatu, Algeria ilirekodi mikasa 97 ya moto ambao ulizuka katika wilaya 16, lakini moto mkali zaidi uliathiri maeneo ya BΓ©jaΓ―a, Bouira na Jijel, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema katika taarifa yake.Β 

Algeria inakabiliwa na wimbi kubwa la joto katika baadhi ya mikoa iliyoathiriwa, na vilele joto ya nyuzi 48 siku ya Jumatatu, ambayo inachangia kukausha mimea, na kuifanya iwe katika hatari zaidi ya milipuko ya moto. Nchini Tunisia, joto limefikia digrii 49.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.