Pata taarifa kuu

Watu 34 wamefariki katika ajali ya barabarani Algeria

Mamlaka nchini  Algeria inasema takriban watu 34 wamefariki katika ajali ya barabarani katika jimbo la kusini la Tamanrasset.

Ajali hiyo imetokea katika jimbo la kusini mwa Tamanrasset
Ajali hiyo imetokea katika jimbo la kusini mwa Tamanrasset RFI
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo imetokea baada ya magari mawili kugongana na  kuwaka moto.Watu wengine 12 wamejuruhiwa.

Eneo la Tamanrasset liko karibu na Niger na Mali.

Timu ya ulinzi wa raia imethibitisha idadi ya vifo na kusema waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.

Watu 34 wamethibitishwa kufariki katika ajali hiyo
Watu 34 wamethibitishwa kufariki katika ajali hiyo © Mamlaka nchini Algeria

Video zilizochapishwa na vyombo vya habari vya ndani, ikiwa ni pamoja na klipu iliyotumwa na Info Trafic Algerie, ilionyesha matokeo ya ajali hiyo na magari kuteketea.

Watu 12 wameripotiwa kujeruhiwa katika ajali hiyo
Watu 12 wameripotiwa kujeruhiwa katika ajali hiyo © Mamlaka nchini Algeria

Ulinzi wa raia ulishiriki picha kadhaa za ajali hiyo huku magari yote mawili yakiwa yameteketea na kuharibiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.