Pata taarifa kuu

Wagner inaendelea na shughuli zake Jamhuri ya Afrika ya Kati

Alexandre Ivanov, mmoja wa maafisa wakuu Wagner na wasaidizi wakuu wa kiongozi wa kundi hilo, amejibu kufuatia "uvumi unaoendelea kuhusu shughuli za kibiashara zinazohusiana na Yevgeny Prigozhin barani Afrika". "Uvumi" kufuatia uasi ulioshindwa wa kundi la wanamgambo dhidi ya Moscow mnamo Juni 24. Katika ujumbe uliotumwa kwenye Telegram, amehakikisha kwamba "kampuni zinazohusiana na uwekezaji wa Urusi zinaendelea kufanya kazi" nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Watu waliovalia sare za kijeshi nje ya makao makuu ya Wagner huko St. Petersburg mnamo Novemba 4, 2022.
Watu waliovalia sare za kijeshi nje ya makao makuu ya Wagner huko St. Petersburg mnamo Novemba 4, 2022. AFP - OLGA MALTSEVA
Matangazo ya kibiashara

Wakati hatima ya Wagner na kiongozi wake Yevgeny Prigozhin ingali kwenye mizani mjini Moscow, kundi la mamluki la Urusi linasema shughuli zake za usalama na kiuchumi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati zinaendelea.

Katika ujumbe uliochapishwa mnamo Julai 17, 2023 kwenye kituo cha Telegram cha Jumuiya ya Maafisa wa Usalama wa Kimataifa (COSI), mmoja wa maafisa wakuu wa Yevgeny Prigozhin anahakikishia kwamba shughuli za kundi la Wagner zinaendelea. Lakini anabainisha kuwa kuna wasiwasi na ukosoaji kwa upande wa mamlaka ya Urusi.

'Ushirikiano wa kampuni za Urusi barani Afrika ndio mafanikio ya Yevgeny Prigozhin'

Alexander Ivanov anasema anataka kujibu maswali mengi anayoulizwa kuhusu "uvumi wa kulazimishwa kuuzwa kwa shughuli za kibiashara zinazohusiana na Yevgeny Prigozhin barani Afrika", hasa "mali zake katika uwanja wa madini". "Natumai hazitathibitishwa au kuathiri uwepo wa Urusi kwenye bara hili," ameandika. "Ushirikiano wa kina wa makampuni ya Urusi barani Afrika ni mafanikio ya Yevgeny Prigozhin, na inaweza kumalizika kwa njia mbaya. Ni mbaya, kwa sababu bado kuna matarajio makubwa, "amesema.

Alexander Ivanov pia anaachia nafasi ya kukosolewa na serikali ya Urusi: "Ninatumai kwamba kongamano lijalo la Urusi na Afrika [lililopangwa mjini Saint-Petersburg Julai 27 na 28] litakuwa halina mvuto na lakini lenye ufanisi zaidi kuliko lile la 2019. "

'Kampuni zinazohusiana na uwekezaji wa Urusi zinaendelea kufanya kazi'

Kuhusiana na Jamhuri ya Afrika ya Kati, mkuu wa COSI anahakikisha kwamba hakuna mabadiliko katika ushirikiano: "Kampuni zinazohusiana na uwekezaji wa Urusi zinaendelea kufanya kazi, miundo ya kibinadamu iliyoundwa na Urusi iko wazi, Nyumba ya Urusi inafanya kazi", akimaanisha taasisi hii ambayo mkurugenzi wake, Dimitri Sityi, mkuu wa shughuli za habari za kundi hilo Bangui, aliondoka Jamhuri ya Afrika ya Kati wiki iliyopita kulingana na Gazeti la Le Monde.

Miongoni mwa kampuni kuu zinazohusishwa na Wagner zinazofanya kazi nchini CAR: uwekezaji wa Lobaye, rasilimali za Midas, Diamville au Bois rouge, hudhibiti sehemu zote za sekta ya dhahabu, almasi na mbao.

Katika ngazi ya usalama, Alexandre Ivanov anathibitisha kwamba "kazi ya wakufunzi inaendelea na wafanyakazi wanaendelea kupishana kama ilivyo nchini humo."

  COSI ilithibitisha mnamo Julai 16 kwamba "wapiganaji mia kadhaa wenye uzoefu" waliwasili Bangui ili kuhakikisha usalama wa kura ya maoni ya Julai 30, habari ambayo haikuweza kuthibitishwa kutoka kwa chanzo huru.

Wiki mbili zilizopita, ripoti zilibaini kwamba mamluki mia kadhaa waliondoka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwa sababu zisizojulikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.