Pata taarifa kuu
UCHUNGUZI-USALAMA

Shinikizo la Urusi barani Afrika: Afrika ya Kati, maabara ya mamluki wa Urusi

Ilikuwa mwishoni mwa mwaka 2017. Kwa kutumia fursa ya kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa, Urusi ilizidi kupata nguvu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kundi la wanamgambo wa Wagner liliingilia kati kulinda utawala dhaifu wa Rais Faustin-Archange Touadéra na kwa haraka kuifanya nchi hii kuwa hifadhi yake, hata kama mapinduzi ya hivi majuzi ya Yevgeny Prigozhin dhidi ya Moscow yanaweza kubadilisha hali ya mambo. 

Jamhuri ya Afrika ya Kati, maabara ya mamluki wa Urusi.
Jamhuri ya Afrika ya Kati, maabara ya mamluki wa Urusi. © Studio graphique FMM
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake ya Julai 13, 2016,mbele ya maafisa wa Ufaransa waliokusanyika katika Hotel de Brienne katika mkesha wa Siku ya Kitaifa, Rais François Hollande alitangaza kumalizika kwa shughuli za kijeshi za jeshi la Ufaransa nchiniJamhuri ya Afrika ya Kati. "Tuliweza kuepusha hatari ya kusambaratika kwa nchi hii. Mafanikio haya yanatufanya tutoe nafasi kwa jumuiya ya kimataifa na mamlaka ya Jamhuri ya Afrika ya Kati," alitangaza François Hollande, ambaye alibainisha: "mwezi Oktoba mwaka uliofuata, Jean-Yves Le Drian, Waziri wa Ulinzi, alikwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati kutangaza rasmi kumalizika kwa Operesheni Sangaris".

Tangazo la kujiondoa kwa jeshi la Ufaransa ilikuwa fursa kwa Moscow, ambayo ilitaka kuongeza ushawishi wake barani Afrika. Kuanzia 2017, Kremlin iliipendekezea Bangui kuwa iko tayari kutoa ulinzi kwa viongozi wa nchi hiyo na kwa usalama wa taifa, anakumbush Thierry Vircoulon, mtafiti katika Taasisi ya Ufaransa ya Uhusiano wa Kimataifa (IFRI). "Suala la uwasilishaji wa silaha lilikuwa lango la Moscow, kwani Jamhuri ya Afrika ya Kati ilikuwa chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa".

'Paris yachukulia vibaya sera ya Urusi'

Ili wanajeshi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (FACA) wapokee silaha, ilibidi idhini kutoka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. "Hapa ndipo Urusi iliingilia kati na kupata, kama mjumbe wa Baraza la Usalama, idhini ya kutoa silaha kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati", anaelezea mtafiti huyu, ambaye anasisitiza kwamba kwa utoaji huu wa silaha, ndipo suala la mafunzo lilianzishwa. "Wakufunzi wa Wagner waliwasili. Ilikuwa ni mshangao: silaha ziliingizwa na kuanza kwa mafunzo”.

Kuwasili kwa Warusi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ilikuwa rahisi mno kwani mnamo 2018, Paris, kama sehemu ya usanifu wake wa usalama, iliomba kuachia ngazi na kutoa nafasi hiyo kwa Moscow. "Kulikuwa na uthamini mbaya wa sera ya Urusi," anaelezea Thierry Vircoulon ambaye "ni wazi kwamba diplomasia ya Ufaransa ilitaka kuendeleza nafasi ya mazungumzo na serikali ya Urusi, bila kujua kuwa serikali ya Urusi, kwa upande wake, haikupendezwa na mazungumzo. Mtafiti anakumbusha kwamba Paris pia ilihusika wakati huo nchini Mali na Operesheni Barkhane, na kwa hivyo haikutaka kuwa msimamizi wa misheni mbili kwa wakati mmoja. Kwa Thierry Vircoulon, Ufaransa "kwa kweli ilijitolea, lazima hilo lisemwe, Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa operesheni nchini Mali".

Wagner hakutimiza mkataba wake wa wa kuleta utulivu Jamhuri ya Afrika ya Kati

Miaka mitano baada ya kuwasili, Warusi wameibadilisha Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwa hifadhi ya kiuchumi, bila kutimiza kikamilifu mkataba wa usalama uliopendekezwa hapo awali.

"Walitimiza kwa sehemu tu", anabainisha Thierry Vircoulon, "kwa kiasi kwamba, kwa kutumwa kwa kundi la wanamgambo la Wagner lenye watu 1,500, waliweza tu kuulinda mji mkuu wa Bangui na baadhi ya miji mikuuu ya mikoa". Mtafiti anatambua kwamba mamluki wa Wagner pia waliweza kutoa mafunzo na kuandaa baadhi ya vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati. "Lakini hawakufanikiwa kuleta utulivu na amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuhakikisha kwamba makundi yenye silaha ambayo yako msituni yanaendelea kujizatiti vilivyo", anasisitiza. Tangu mwisho wa 2021, mamluki wa Wagner wameshindwa na makundi haya yenye silaha katika maeneo mengi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Je, kundi la Wagner litasalia nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati au Rais Faustin-Archange Touadéra atatafuta uungwaji mkono mwingine? Siku chache kabla ya mkutano wa 2 wa kilele wa Urusi na Afrika huko Saint Petersburg, chaguzi zote ziko mezani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.