Pata taarifa kuu

Mamluki wa Wagner waanza kuondoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui yakanusha

Idadi isiyojulikana ya mamluki kutoka kundi la wanamgambo wa Urusi la Wagner waliondoka Jamhuri ya Afrika ya Kati katika siku za hivi karibuni, kulingana na vyanzo kadhaa vya kigeni, habari zilizokanushwa vikali na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Picha hii isiyo na tarehe iliyotolewa na jeshi la Ufaransa inaonyesha mamluki watatu wa Urusi, kaskazini mwa Mali.
Picha hii isiyo na tarehe iliyotolewa na jeshi la Ufaransa inaonyesha mamluki watatu wa Urusi, kaskazini mwa Mali. AP
Matangazo ya kibiashara

"Kuna mamluki wa Wagner ambao wameondoka nchini Jamhuri ya afrika ya Kati. Pengine ni mchanganyiko wa matatizo ya sasa ya Wagner na pesa zisizotosha kutoka kwa Rais Faustin-Archange Touadéra", chanzo kutoka Ufaransa kilicho karibu na faili hii kimeliambia shirika la habari la AFP.

Hadhi ya kampuni ya kibinafsi ya kijeshi na kiongozi wake Yevgeny Prigozhin haina uhakika zaidi kuliko hapo awali tangu uasi wake wa uliyositishwa nchini Urusi mnamo Juni 23 na 24. Operesheni hiyo iliwachukua mamluki hao hadi kilomita mia chache kutoka Moscow kabla kusitisha maandamano hayo, chini ya masharti ya makubaliano na Rais wa Urusi Vladimir Putin, ambayo maelezo yake hayajajulikana.

Lakini uingiliaji kati wake nje ya nchi, hasa nchini Syria na katika nchi kadhaa za Afrika (Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, hasa Mali) hadi sasa haujatiliwa shaka hadharani. Mara tu uasi ulipotangazwa kumalizika, Bangui ilithibitisha kwamba shughuli za Wagner 'zitaendelea'.

"Urusi imeingia kandarasi ndogo na Wagner, ikiwa Urusi haikubaliani tena na Wagner basi itatutumia kikosi kipya," Fidèle Gouandjika, waziri mshauri maalum wa Rais Touadera, ameliambia shirika la habari la AFP.

"Tuna safari nyingi za ndege, nafasi ambazo zimeachwa. Sina orodha kwa kila kitengo lakini tumeona orodha ya ndege ambazo zimeruka, ikiwa ni pamoja na Ilyouchine-76", ndege ya usafirishaji ya askari wa Urusi, chanzo cha usalama cha kigeni kimeliambia shirika la habari cha AFP.

Aina hii ya ndege imekuwa ikitumika mara kwa mara tangu mwka 2018 kuwasafirisha wanamgambo wa Wagner kwenda na kutoka Bangui. "Kinachozunguka kina msingi mzuri," kimeongeza chanzo hicho cha kigeni. "Pia tunaangalia kinachoendelea nchini Mali lakini katika hatua hii, hatuoni chochote".

Alipoulizwa na AFP, Fidèle Gouandjika, hata hivyo, alikanusha habari hii Ijumaa. "Hakuna wanajeshi wa Urusi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wanaoondoka kwenda nchi ya kigeni, wote wapo kwenye eneo hilo na kile kinachosemwa na vyombo vya habari ni madai ya uwongo tu," amesema.

Chanzo cha usalama cha Ufaransa kwa upande wake kimethibitisha kuondoka kwa wanamgambo hao kwa "kutokuwa na uhakika juu ya malipo ya mishahara katika miezi ijayo na wasiwasi juu ya uwezekano wa kulipiza kisasi kwa familia za mamluki ambao wataendelea kujiunga na Wagner". Kulingana na chanzo hiki, wanamgambo hao wamepewa chaguo kati ya kurudi kwa maisha ya kiraia, kuandikishwa katika jeshi la Urusi au kuandikishwa katika kampuni zingine za kibinafsi za Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.