Pata taarifa kuu

Totalenergies yarejelea shughuli zake nchini Msumbiji

Nairobi – Baada ya kuwa imesitisha shughuli za uchimbaji mafuta katika pwani ya nchi ya Msumbiji tangu mwaka 2021 kutokana na uvamizi wa makundi ya kijihadi kwenye mji wa Cabo del gado, kampuni ya Totalenergies, sasa imerejea tena shughuli zake kwenye eneo hilo.

TotalEnergies imeanza kurejelea shughuli zake nchini Msumbiji baada ya kusitishwa mwaka wa 2021
TotalEnergies imeanza kurejelea shughuli zake nchini Msumbiji baada ya kusitishwa mwaka wa 2021 AP - Michel Spingler
Matangazo ya kibiashara

Wakati huu hali ya usalama ikianza kurejea kawaida, kampuni hiyo nayo imeanza kurejesha baadhi ya operesheni zake, ikiwa na imani kuwa hadi kufikia mwaka 2027, itakamilisha kuchakata gesi kwenye êneo hilo.

Licha ya kuwa wapiganaji wa Al Shabaab, wamepunguza mashambulio, bado uwepo wa kundi hilo kwanye mpaka wa nchi hiyo na Tanzania umeripotiwa, wakati huu mji mkuu wa êneo hilo Mochimboa Da Praia ukikombolewa na vikosi vya Serikali kwa kushirikiana na vile vya Rwanda.

Hata hivyo licha ya viongozi kwenye êneo hilo kuthibitisha usalama kurejea katika hali ya kawaida, kampuni ya Total haijatoa tarifa rasmi kueleza ni lini hasa itarejelea shughuli kamili, ingawa mkandarasi Wake tayari amezana shughuli za awali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.