Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

Viongozi wawili wa upinzani waachiliwa Tunisia

Wapinzani wawili mashuhuri wa Rais wa Tunisia, Kais Saied, waliofungwa jela kwa zaidi ya miezi mitano, waliachiliwa huru usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa, lakini wanasema wana wasiwasi kuhusu wenzao ambao bado wanazuiliwa.

Alipotoka jela, Chaïma Issa, ambaye alikuwa amevalia fulana nyekundu iliyoandikwa neno "kuwa huru", amesema ana "furaha ya kuwa huru".
Alipotoka jela, Chaïma Issa, ambaye alikuwa amevalia fulana nyekundu iliyoandikwa neno "kuwa huru", amesema ana "furaha ya kuwa huru". © AFP
Matangazo ya kibiashara

Chaima Issa, mwanasiasa wa muungano mkuu wa upinzani wa National Salvation Front (FSN), na waziri wa zamani Lazhar Akremi ni miongoni mwa kundi la wapinzani wapatao 20 na wafanyabiashara waliokamatwa tangu mwezi Februari katika sehemu ya uchunguzi wa "njama dhidi ya usalama wa taifa". Bw Saied aliwaita "magaidi" lakini mawakili wao walikashifu faili za mashitaka zilizo 'tupu'.

Alipotoka jela, Chaïma Issa, ambaye alikuwa amevalia fulana nyekundu iliyoandikwa neno "kuwa huru", amesema anafurahia "kuona yuko huru". "Lakini ni furaha isiyokamilika" kwa sababu "udhalimu nilioupata bado unawakumba marafiki zangu" ambao bado wamefungwa, amesema katia mkutano na waandishi wa habari.

“Tuliingia, tumeondoka. Hatujui kwanini tuliiingia jela, hatujui kwanini tume'achiliwa huru, amesema Bw. Akremi.

Kamati ya utetezi, ambayo imetangaza uamuzi wa kuachiliwa kwao, imesema inaomba kuachiliwa kwa wapinzani wengine wa kisiasa, lakini jaji wa Mahakama ya Rufaa alikataa ombi hili.

Kabla yao, mnamo Mei 24, bosi wa Mosaïque FM, kituo cha redio cha kibinafsi kinachosikilizwa zaidi nchini Tunisia, Nouredine Boutar, aliachiliwa baada ya kufungwa kama sehemu ya uchunguzi huu, lakini kwa masharti ya kulipa dhamana ya milioni moja. dinari (karibu euro 300,000). Anaendelea kufunguliwa mashtaka kwa kula njama dhidi ya usalama wa serikali na utakatishaji fedha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.