Pata taarifa kuu

Sudan: Zaidi ya watu milioni tatu wametoroka makazi yao

Zaidi ya watu milioni tatu wametoroka makazi yao nchini Sudan, ambako vita vimekuwa vikiendelea kwa muda wa miezi mitatu, amesema mjumbe wa Umoja wa Mataifa, ambaye amepoteza imani kwa Khartoum, akitoa wito kwa majenerali wawili walioanzisha uhasama "kuchukuliwa hatua zinafaa" kwa kurejesha utulivu.

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan (kushoto) na Jenerali Mohamed Hamdan Daglo almaarufu Hemedti (kulia).
Jenerali Abdel Fattah al-Burhan (kushoto) na Jenerali Mohamed Hamdan Daglo almaarufu Hemedti (kulia). © AP Photo - Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya watu ambao wamekimbilia nje ya nchi kutokana na mapigano nchini Sudan ni karibu 724,000 huku idadi ya wakimbizi wa ndani ikizidi milioni 2.4, kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).

"Hawa ni watu ambao walikata tamaa, ambao wamekimbia wakihofia usalama wao, familia ambazo zimetenganishwa na watoto ambao hawataweza tena kwenda shule," mmoja wa wasemaji wa shirika hili la Umoja wa Mataifa, Safa Msehl, amesema.

Vita visivyo na huruma vya kuwania madaraka kati ya jeshi, linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah, na wanamgambo wa Rapid Support Forces (FSR) wanaoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdane Daglo pia vimesababisha karibu vifo 3,000 tangu Aprili 15.

Katika uwanja wa vita, mapigano yanaendelea bila kukoma, hasa huko Khartoum, ambapo mamilioni ya wakaazi bado wamekwama, huku wakikabiliwa na uhaba wa maji na kukosa umeme na wakikabiliwa na  joto kali.

Mji mkuu ulilengwa tena na mashambulizi ya anga siku ya Jumatano, mashahidi wamesema wakinukuliwa na shirika la habari la AFP, mmoja wao akiripoti "ndege zilizoshambulia vituo vya RSF tangu alfajiri".

Mashambulizi ya anga yameongezeka hivi karibuni, na kuua makumi ya raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.