Pata taarifa kuu

Mjini Khartoum, vita vikali vyarindima kwenye makao makuu ya polisi

Jeshi la Sudan limejikuta katika matatizo likikabiliana na makundi kadhaa kwenye katika maeneo kadhaa siku ya Jumatatu: mjini Khartoum, wanamgambo wa RSF wamechukuwa udhibiti wa makao makuu ya polisi na kukamata silaha za jeshi la serikali na kusini kwenye mpaka na Ethiopia, kundi la waasi limeanzisha mapigano mapya dhidi ya jeshi.

Shirika lisilo la kiserikali la Acled linahesabu zaidi ya watu 2,800 waliofariki katika vita nchini Sudan, idadi ambayo kwa kiasi kikubwa haikukadiriwa.
Shirika lisilo la kiserikali la Acled linahesabu zaidi ya watu 2,800 waliofariki katika vita nchini Sudan, idadi ambayo kwa kiasi kikubwa haikukadiriwa. REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Jumapili jioni, baada ya miezi miwili na nusu ya vita dhidi ya jeshi linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (FSR) walitangaza katika taarifa "ushindi katika vita vilvyotokea kwenye makao makuu ya polisi". Na Jumatatu asubuhi, wakaazi wa mji wa Kurmuk, kwenye mpaka na Ethiopia, waliripoti kwa shirika la habari la AFP kwamba kundi la waasi lilianzisha mashambulizi dhidi ya jeshi.

Tukio hilo linaripotiwa wakati kikosi cha RSF kinajaribu kuimarisha nafasi yake kwenye mapigano makali dhidi ya jeshi la taifa hususani kwenye viunga vya mji mkuu wa Khartoum.

Kundi hili lilianzisha mapigano mapya siku ya Alhamisi huko Kordofan Kusini, inayopakana na Sudan Kusini, na kulazimisha jeshi kujibu pande tofauti, zote Kusini. Hata hivyo, afisa wa zamani wa jeshi kwa sharti la kutotajwa jina amelielezea shirika la habari la AFP, kutekwa kwa makao makuu ya polisi - kwenye ukingo wa kusini mwa mji mkuu - kunabadilisha hali ya mambo kwa kiasi kikubwa.

"Tuna udhibiti kamili wa Makao Makuu(...) na tumekamata idadi kubwa ya magari, silaha na risasi", inabainisha FSR, ikibaini kukamatwa kwa magari ya kijeshi (pick-up), magari ya kivita na vifaru.

Udhibiti na Tishio

Kutekwa kwa makao makuu ya polisi, kama hali haitabadilika, "itakuwa na athari kubwa kwenye vita vya Khartoum", ameongeza afisa huyo kwani "amehakikisha vikosi vya FSR  miechukuwa udhibiti wa mlango wa kusini wa mji mkuu" .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.