Pata taarifa kuu

Sudan: Baraza Kuu laomba msaada kutoka Moscow kupatanisha katika mgogoro

Makamu wa rais wa Baraza Kuu nchini Sudan, Malik Agar, alikuwa Moscow ambapo alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov. Aliomba usaidizi wa Moscow katika kupatanisha mgogoro wa Sudan. Vita vinaripotiwa kati ya wanajeshi na wanamgambo nchini Sudan tangu Aprili 15. Katika mkutano na waandishi wa habari, Malik Agar alibaini mtazamo wa jeshi katika mapambano haya na pia mapngo unaowezekana wa kuondokana na mzozo huo.

Malik Hagar (G) aux côtés du général Mohamed Hamdan Daglo, dit Hemedti, en 2019.
Malik Hagar (G) aux côtés du général Mohamed Hamdan Daglo, dit Hemedti, en 2019. AFP - AKUOT CHOL
Matangazo ya kibiashara

 

Kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Moscow iko tayari kabisa kuchukua jukumu hili la upatanishi, baada ya Saudi Arabia na Marekani kushindwa kwa upatanishi. Hii itaiwezesha Moscow kurejea katika masuala ya Afrika ili kujaribu kuhifadhi maslahi yake nchini Sudan na ushawishi wake ambao umepungua tangu kuanguka kwa utawala wa Omar al-Bashir mwaka 2019.

Kulingana na wataalamu kadhaa, Moscow ina uwezo wa moja kwa moja kuingilia kati kama mpatanishi katika mgogoro huu. Mbali na kuwa mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Moscow imeweza kudumisha uhusiano mzuri sana na pande mbili zinazo kinzana na na nchi nyingi jirani za Sudan.

Malik Agar alikumbusha umuhimu wa uhusiano wa kihistoria lakini pia wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili na mkuu wa diplomasia ya Urusi alisisitiza juu ya haja ya kuhuisha uhusiano wao wa pande mbili.

Kwa muda mrefu, Sudan kituo muhimu kwa Moscow katika Afrika, daraja la kueneza ushawishi wake katika bara hili. Hatimaye, muda wa ziara hii unaonekana kuwa muhimu, unakuja wakati Khartoum pia inataka kuwajumuisha wanamgambo wake katika jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.