Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Milipuko yasikika Khartoum siku ya kwanza ya Eid

Mamia ya watu waliomba amani katika ibada yao siku ya Jumatano huko Khartoum siku ya kwanza ya Eid al-Adha, sherehe kuu ya Waislamu, lakini milio ya risasi na milipuko vimetikisa tena mji mkuu wa Sudan.

Waislamu wa Sudan ambao walikimbia vurugu huko Khartoum, hukusanyika kwa sala ya asubuhi ya Eid al-Adha mnamo Juni 28, 2023, katika mkoa wa Jazira, kusini mwa Khartoum.
Waislamu wa Sudan ambao walikimbia vurugu huko Khartoum, hukusanyika kwa sala ya asubuhi ya Eid al-Adha mnamo Juni 28, 2023, katika mkoa wa Jazira, kusini mwa Khartoum. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Majenerali wawili ambao wanahasimiana tangu katikati ya mwezi Aprili katika mji mkuu wa Sudan na katika mkoa wa Darfur (Magharibi), siku ya Jumanne walitangaza kila moja kwa upande wake kusitisha mapigano siku ya Eid lakini, kama ilivyokuwa hapo awali, usitishwaji mapigano haujatekelezwa.

Mchana, wakaazi wa Omdourman, kitongoji cha kaskazini mwa jiji, waliripoti "shambulio la angani naurushaji wa makombora yaliripotiwa", wakati kwa siku kadhaa, vikosi vya msaada wa haraka (FSR, paramilitaries) vya Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, vinajaribu kuteka mji mkuu.

Katika hotuba kwa taifa siku ya Jumanne, kwenye hafla ya Eid, mkuu wa jeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, aliwaita wale wote waliomtaka, pamoja na vijana, ili wajiunge na kambi yake. Wito uliofutiliwa mbali na raia, ambao wamechoka na mzozo ambao umebadilisha miji yote kuwa maeneo ya vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.