Pata taarifa kuu

Maandamano dhidi ya wapenzi wa jinsia moja yafanyika nchini Malawi

Takriban watu 5,000 wameshiriki katika maandamano dhidi ya watu kutoka jamii ya wapenzi wa jinsia moja, LGBTQ, siku ya Alhamisi huko Lilongwe, mji mkuu wa Malawi, nchi ya kihafidhina kusini mwa Afrika ambako uhusiano wa jinsia moja ni kinyume cha sheria.

Maandamano ambayo yameandaliwa na Kanisa Katoliki nchini Malawi na kuungwa mkono na makundi mengine ya kidini, maandamano pia yamefanyika wakati huo huo katika miji mingine mikubwa nchini Malawi, ikiwa ni pamoja na Blantyre, Mzuzu na Zomba.
Maandamano ambayo yameandaliwa na Kanisa Katoliki nchini Malawi na kuungwa mkono na makundi mengine ya kidini, maandamano pia yamefanyika wakati huo huo katika miji mingine mikubwa nchini Malawi, ikiwa ni pamoja na Blantyre, Mzuzu na Zomba. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Maandamano ambayo yameandaliwa na Kanisa Katoliki nchini Malawi na kuungwa mkono na makundi mengine ya kidini, pia yamefanyika wakati huo huo katika miji mingine mikubwa nchini Malawi, ikiwa ni pamoja na Blantyre, Mzuzu na Zomba. Waandamanaji mjini Lilongwe waliongozwa na Askofu Mkuu Desmond Tambala. Walitembea jijini wakiwa wamebeba mabango kabla ya kuwasilisha ombi kwa wabunge mbele ya makao makuu ya bunge.

Ushoga ni kinyume na kila kitu tunachoamini kama watu," Sheikh Dinala Chabulika wa Jumuiya ya Waislamu wa Malawi amesema alipokuwa akisoma masharti ya ombi hilo. Mchungaji William Tembo wa Baraza la Makanisa la Malawi amesema uhusiano wa watu wa jinsia moja ni "ajabu": "Hatuko tayari kukubali matukio haya yasiyojulikana nchini Malawi," amesema.

"Sisi ni taifa lenye mwelekeo wa familia, taifa linalomcha Mungu na ndiyo maana kanisa linapinga mahusiano ya jinsia moja," ameongeza.

Waandamanaji walimtaka Rais Lazarus Chakwera, mhubiri wa zamani wa injili kupinga shinikizo la kuhalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja. Msemaji wa serikali Moses Kunkuyu amewaambia waandamanaji kwamba utawala utazingatia wasiwasi uliotolewa na viongozi wa kidini.

Maandamano hayo yaliambatana na kesi katika Mahakama ya Kikatiba iliyoletwa na Jan Willem Akstar, mfanyakazi wa shirika lisilo kuwa la serikali kutoka Uholanzi, na Jana Gonani, aliyebadili jinsia. Wanandoa hao wanataka kufutwa kwa marufuku ya ndoa za jinsia moja na uhusiano wa jinsia moja, wakijadili pamoja na mambo mengine kuwa ni ukiukwaji wa haki binafsi na utu.

Mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja ni kosa la jinai nchini Malawi linaloadhibiwa kwa hadi miaka 14 jela. Akstar na Gonani walishtakiwa tofauti chini ya sheria ya enzi ya ukoloni inayokataza kulawiti.

Bi Gonani alihukumiwa kifungo cha miaka minane gerezani mwaka wa 2021 na Bw Akstar, 51, kwa sasa anakabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji wa kingono. Kesi zao zimeunganishwa mbele ya mahakama ya kikatiba, ambayo inatarajiwa kuanza kusikilizwa wiki ijayo.

Wizara ya Sheria ya Malawi ilitoa amri ya kusitisha kukamatwa na kufunguliwa mashitaka kwa vitendo vya ushoga vilivyokubaliwa mwaka 2012, lakini amri hiyo ilikataliwa na Mahakama Kuu mwaka 2016 ikisubiri mapitio ya mahakama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.