Pata taarifa kuu

Jamhuri ya Afrika ya Kati: Rasimu ya Katiba mpya yachukua hatua mpya

Kura ya maoni kuhusu rasimu ya Katiba mpya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, imepangwa katika muda wa wiki mbili tu, tarehe 30 Julai na, kwa kuzingatia uchaguzi huu, Rais Faustin-Archange Touadéra amewasilisha rasimu yanakala hii kwa uongozi wa taifa wa kampeni ya kura ya maoni - chombo kinachohusika na kuchapisha maandishi haya. Hatua hiyo kuu inahusu muhula wa rais, ambao unatoka miaka mitano pekee kwa mihula miwili hadi miaka saba bila kikomo.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra, wakati wa hafla ya mwaka mmoja ya muhula katika Bunge la taifa, mjini Bangui mnamo Machi 30, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra, wakati wa hafla ya mwaka mmoja ya muhula katika Bunge la taifa, mjini Bangui mnamo Machi 30, 2022. © Barbara Debout / AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Bangui, Rolf Stève Domia-leu

Rasimu ya nakala inajumuisha mabadiliko kadhaa muhimu ikilinganishwa na nakala ya sasa inayotumika tangu mwaka 2016.

Ibara ya 67 inaruhusu "rais kutawala milele", kulingana na wapinzani wa mageuzi haya. Rais Touadéra pia ataweza kugombea tena uchaguzi mwaka 2025. Na ili kushindana katika uchaguzi ujao, itakuwa muhimu pia kuwa na uraia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati pekee. Uraia pacha utapigwa marufuku na kifungu cha 10, isipokuwa ikiwa bunge litapinga hili.

Mswada huu pia unatoa mageuzi ya kina ya Mahakama ya Katiba. Hakika, katika nakala ya sasa, sita kati ya majaji tisa wanachaguliwa ndani ya mfumo wa kisheria na usawa wa kijinsia ni lazima, hali ambayo inahakikisha uhuru fulani kwa majaji hawa.

Kuanzia sasa kutakuwa na majaji kumi na moja katika mahakama hii, watatu kati yao wanateuliwa na Mkuu wa Nchi na watatu wanateuliwa na spika wa Bunge.

Mswada huu utawasilishwa wakati wa kampeni ya kura ya maoni iliyopangwa Julai 15 hadi 28, na kura ya maoni imepangwa kufanyika Julai 30.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.