Pata taarifa kuu

Sudan: Mashambulio dhidi ya ofisi za balozi za kigeni yakashifiwa

NAIROBI – Mashambulio na uporaji katika majengo ya balozi za kigeni nchini Sudan yamendelea kuripotiwa wakati huu Algeria ikiwa nchi ya hivi punde kulaani matukio hayo.

Wapiganaji wa RSF wamekuwa wakituhumiwa kwa kutekeleza mashambulio dhidi ya ofisi za balozi za kigeni
Wapiganaji wa RSF wamekuwa wakituhumiwa kwa kutekeleza mashambulio dhidi ya ofisi za balozi za kigeni © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Jumatano ya wiki hii, wizara ya mambo ya kigeni ya Algeria ilisema kwamba makao ya balozi wake nchini Sudan yalishambuliwa na kuporwa siku iliyotangulia.

Mamlaka nchini Sudan imetakiwa kuchukua jukumu la kuwalinda raia wa kigeni kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Kando na Algeria, Zimbabwe nayo imelaani shambulio kwenye ubalozi na mwaikilishi wake mjini Khartoum, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa Zimbabwe akiwatuhumu wapiganaji wa with Rapid Support Forces (RSF) kwa kuhusika na shambulio hilo .

"Tuna taarifa kwamba sehemu kubwa ya majengo ya raia wa kigeni yalilengwa, kutumia mapigano kwa ajili ya kupora mali ya wajumbe wetu na ubalozi wetu huko ni makosa," Livit Mugejo alisema.

Jumanne ya wiki hii, Mauritania ilisema ubalozi wake mjini Khartoum nao pia ulishambuliwa na kuporwa na watu wenye silaha.

Vyombo vya habari nchini Mauritania viliripoti kwamba karibia magari matatu yanayotumika na balozi wake na wafanyikazi wake yaliibiwa.

Jeshi la Sudan limeendelea kuwalaumu wapiganaji wa RSF kwa kutekeleza mashambulio katika ofisi za ubalozi wa kigeni, madai ambayo RSF imekanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.