Pata taarifa kuu

Ukuaji ukanda wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara unaendelea kupungua

Haya ni maoni yaliyotolewa na Benki ya Dunia. Taasisi ya kifedha ilichapisha, Jumanne, Juni 7, mtazamo wake wa kiuchumi duniani. Picha inayotolewa ni ya kusikitisha. Matarajio ya kupunguza umaskini ni madogo. Hali hii inaweza kuelezewa na angalau mambo mawili.

Luanda, mji mkuu wa Angola.
Luanda, mji mkuu wa Angola. Benjamin SHEPPARD / AFP
Matangazo ya kibiashara

Sababu ya kwanza iliyoangaziwa na Benki ya Dunia: mfumuko wa bei unaoenda kasi. Ingawa imepungua, kupanda kwa kila mwaka kwa bei ya chakula kunasalia katika tarakimu mbili katika 70% ya nchi. Tatizo ni gharama kubwa za pembejeo za kilimo, kushuka kwa thamani ya sarafu na matatizo mapya ya usambazaji yanayohusishwa na vurugu za kikabila au mabadiliko ya tabia nchi.

Kulingana na benki hiyo, matukio haya yamezidisha umaskini na uhaba wa chakula ikilinganishwa na mwanzo wa mwaka 2022. Kwa hivyo Benki ya Dunia inahesabu watu milioni 35 wa ziada walio katika hali ya uhaba mkubwa wa chakula.

Jambo la pili lililoangaziwa: ukuaji wa uchumi wa nchi tatu kubwa zaidi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara unaendelea kupungua. Afŕika Kusini inaendelea kuadhibiwa na kukatika kwa umeme kwa kiasi kikubwa, pamoja na mfumuko wa bei na kubana kwa seŕa za ndani. Nchini Angola na Nigeria - wazalishaji wakubwa wa mafuta katika Afrika - kasi ya ukuaji imekwama, Benki ya Dunia inaendelea, kutokana na kushuka kwa bei ya nishati.

Ukuaji katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara unapaswa kuendelea kupungua hadi 3.2% katika 2023. Kupanda hadi 3.9% kunatarajiwa katika 2024.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.