Pata taarifa kuu

Pembe ya Afrika: Mkuu wa Umoja wa Mataifa ahimiza ulimwengu kuzuia njaa

Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Jumatano amehimiza ulimwengu kuzuia 'watu kufariki' kwa njaa katika Pembe ya Afrika iliyokumbwa na ukame mkubwa kutokana na 'machafuko ya tabia nchi'.

Watu waliokimbia makazi yao kutokana na mzozo wa Tigray wanakusanyika katika eneo la Afar, nchini Ethiopia.
Watu waliokimbia makazi yao kutokana na mzozo wa Tigray wanakusanyika katika eneo la Afar, nchini Ethiopia. © UNHCR/Alessandro Pasta
Matangazo ya kibiashara

Katika ufunguzi wa mkutano wa wafadhili wa ukanda huu wa Afrika Mashariki mjini New York (Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Kenya na Sudan), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa "jumuiya ya kimataifa kufadhili haraka programu za kibinadamu kwa 2023".

Kwa sauti kubwa, katika hotuba ya kuunga mkono nchi zinazoandaa mkutano huu (Italia, Qatar, Uingereza, Marekani), Bw. Guterres amesema "haikubaliki" kwamba "hadi sasa, ni karibu 20% tu ya pesa ambazo zimetolewa".

Kulingana na takwimu za umma kutoka kwa huduma za kifedha za Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA), kati ya dola bilioni saba zinazotarajiwa mwaka 2023, dola bilioni 1.63 (au 23%) hadi sasa zimeahidiwa.

'Watu watakufa'

"Bila ya msaada mkubwa na wa haraka wa pesa, shughuli za dharura zitasimama na watu watafariki," Guterres ameonya.

"Tunapaswa kuchukuwa hatua sasa ili kuzuia mzozo usigeuke kuwa janga", amebainisha mkuu wa Umoja wa Mataifa, akisema kuwa mnamo 2022 nchi wafadhili za Pembe ya Afrika ziliwezesha "kupeleka msaada wa dharura kwa watu milioni 20 na kusaidia kuzuia njaa. ".

Kwa Somalia pekee, katibu mkuu alinukuu takwimu kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa ya WHO na UNICEF ​​​​ambayo yanabaini kwamba"mwaka jana, ukame uligharimu maisha ya watu 40,000, nusu yao wakiwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5".

Na katika nchi hii ya Afrika Mashariki, tangu mwanzoni mwa 2023, zaidi ya watu milioni moja wamekimbia makazi yao kutokana na vita, mafuriko au ukame, na kuongeza hatari ya njaa.

Nchini Somalia, nchi yenye wakazi wapatao milioni 17, zaidi ya milioni 3.8 wameyakimbia makazi yao "kuja kuzidisha hali mbaya ya kibinadamu ambayo tayari ni mbaya ambapo watu milioni 6.7 wanatatizika kukidhi mahitaji yao ya chakula", amesisitiza katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa mashirika hayo mawili ya kibinadamu. .

Zaidi ya watoto nusu milioni wanakabiliwa na utapiamlo mkali, kulingana na mashirika hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.