Pata taarifa kuu

Sudan: Pande zinazokinzana zakubaliana kusitisha mapigano kwa siku saba

Wawakilishi wa jeshi la Sudan, wakiongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, na wanamgambo wa kikosi cha Rapid Support Forces (RSF), wa Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, wamekubaliana kusitisha mapigano kwa wiki moja, kuanzia Jumatatu, Marekani na Saudi Arabia zilitangaza katika taarifa ya pamoja siku ya Jumamosi.

Wanajeshi wa jeshi la Sudan wakiwa wamesimama karibu na gari kwenye barabara iliyofungwa mjini Khartoum Mei 20, 2023.
Wanajeshi wa jeshi la Sudan wakiwa wamesimama karibu na gari kwenye barabara iliyofungwa mjini Khartoum Mei 20, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko New York, Loubna Anaki

Mpango huo ulitangazwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka vinaahidi kusitisha mapigano kwa muda. Usitishaji mapigano ambao utaanza kutumika Jumatatu hii kuanzia 9:45.

Kwa mujibu wa Washington, pande hizo mbili pia zimeahidi kutozidisha mapigano yao ifikapo Jumatatu jioni. Pia waliahidi kuwezesha utoaji na usambazaji wa misaada ya kibinadamu, na kuondoa askari wao kutoka hospitali na majengo ya huduma za umma. Ahadi zinazofanana na zile zilizotolewa hapo awali, lakini makubaliano ya usitishaji mapigano yaliopita hahayajawahi kuheshimiwa, wala si na jeshi la Sudan, wala na vikosi vya msaada wa Haraka.

Katika kutangaza makubaliano haya mapya, maafisa wa Marekani wanabaini wazi kuwa huu sio mwanzo wa mchakato wa kisiasa au mazungumzo. Hata inabainisha kwamba Riyadh na Washington zitaendelea na juhudi zao za kujaribu kuiondoa Sudan katika mgogoro huo.

Mzozo wa Sudan ulikuwa katikati ya majibu ya kidiplomasia wiki hii na mjumbe maalum wa Rapid Support Forces Yousif Izzat. Mjumbe wa Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, anayejulikana kwa jina la Hemedti, amezuru Juba siku ya Jumatano, ambapo alikutana na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir. Katika mchakato huo, alikutana na mkuu wa taifa wa Uganda Yoweri Museveni, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari vya FSR iliyochapishwa Jumamosi. Jenerali Abdel Fattah al-Burhan haungi mkono mikutano kama hii.

Kwa upande wa Sudan Kusini, Khartoum ilitoa malalamiko rasmi. Katika barua ya kidiplomasia iliyotumwa Juba siku ya Alhamisi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan ilieleza kutokubaliana kwake baada ya ziara ya mjumbe maalum wa vikosi vya Msaada wa Haraka, RSF vya Jenerali Mohamed Hamdane Daglo.

Jenerali al-Burhan ana wasiwasi kuhusu upendeleo wa Sudan Kusini, mpatanishi katika mzozo huo dhidi ya wanamgambo.

Juba inajitetea. "Katika upatanishi, unapaswa kukutana na pande zote, kwa usawa," imesema Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan Kusini.

Ziara hii ilimuwezesha Yousif Izzat kukutana na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na wawakilishi kadhaa wa shirika la kikanda la IGAD. Mwishoni mwa mkutano wake, alisema yuko tayari kushiriki katika juhudi zote za Sudan Kusini kuendeleza amani nchini Sudan. Nchini Uganda, mjumbe maalum wa vikosi vya Msaada wa Haraka, pia alisisitiza kujitolea kwa FSR kwa ajili ya amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.