Pata taarifa kuu

Juba kuwahamisha maelfu ya wakimbizi kutoka nchini Sudan

NAIROBI – Mamlaka nchini Sudan Kusini, zinapanga kuwahamisha wakimbizi wanaoingia nchini humo kutokea Sudan, kwa lengo la kuwatafutia sehemu kubwa zaidi kaskazini mwa mji wa Bahr El Ghazal.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa waziri anayehusika na masuala ya kibinadamu Sudan Kusini, Albino Akol Atak, amesema hatua hii inatokana na ongezeko kubwa la watu wanaoomba hifadhi kukimbia mapigano.

Ardhi yetu inatarajia kutoa hifadhi ya kwa idadi kubwa ya wakimbizi wanaoingia, na sio tu kwa takwimu zilizopita lakini kwa makadirio sio chini ya elfu hamsini.

00:27

Waziri wa Sudan Kusini, Albino Akol Atak kuhusu wakimbizi wa Sudan

Haya yanajiri wakati huu rais wa Kenya William Ruto akiwa kiongozi wa hivi punde kuwaomba majenerali wanaopigana nchini Sudan, kuacha mapigano na kutaka kutafakari upya kwa Umoja wa Afrika (AU) ili kushughulikia vyema migogoro barani humo.

Rais wa Kenya, William Ruto akiwa nchini Afrika Kusini, Mei 17, 2023.
Rais wa Kenya, William Ruto akiwa nchini Afrika Kusini, Mei 17, 2023. © WilliamsRuto

Takriban watu 1000 wameuawa huku wengine milioni moja wakifanywa wakimbizi nchini Sudan, tangu kuzuka kwa mgogoro kati ya mkuu wa jeshi jenerali Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake Mohamed Hamdan Daglo, ambaye pia ni kiongozi wa kundi la RSF.

Tunahitaji kuwaambia majenerali hawa kuacha ukatili huu, Ruto ameuambia mkutano wa wabunge nchini Afrika Kusini.

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya dola bilioni tatu zinahitajika ili kutoa msaada wa dharura kwa taifa hilo, na matumaini ya kumalizika kwa vita ni changa, baada ya majenerali hao kutoheshimu makubaliano ya hapo awali ya kusitisha mapigano ndani ya wiki kadhaa zilizopita.

Ruto akihutubia mkutano huo wa wabunge nchini Afrika Kusini, amesema hali hii nchini Sudan, inaonyesha wazi mapungufu ya Afrika.

Rais wa Kenya William Ruto akihutubia Mkutano wa Wabunge wa Afrika nzima, mkutano wa Wabunge wa AU karibu na Johannesburg Mei 17, 2023.
Rais wa Kenya William Ruto akihutubia Mkutano wa Wabunge wa Afrika nzima, mkutano wa Wabunge wa AU karibu na Johannesburg Mei 17, 2023. © WilliamsRuto

Rais huyo amesema muda umefika wa kutafakari iwapo Umoja wa Mataifa utaunda kamati ya Amani na Usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.