Pata taarifa kuu

Watu 16 wameuawa katika mapigano ya kikabili kusini mwa Sudan

NAIROBI – Mamlaka kusini mwa Sudan, imetangaza makataa ya watu kutembea nje usiku baada ya watu karibia 16 kuuawa katika mapigano ya kikabila wengine wakiwa wamejuruhiwa.

Mapigano ya kikabila yamesababisha vifo vya watu 16 kusini mwa Sudan
Mapigano ya kikabila yamesababisha vifo vya watu 16 kusini mwa Sudan Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la SUNA, Mapigano hayo yaliaanza siku ya Jumapili kati ya makabila ya Hausa na Nuba katika eneo la Kosti, mji mkuu wa jimbo la White Nile mpaka na Sudan Kusini.

Mapigano haya yanakuja wakati huu pia makabiliano kati ya wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa RSF yakiwa yanaendelea tangu Aprili 15, karibia watu 750 wakiwa wamepoteza maisha.

Hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka kati ya makundi hayo mawili ya kikabila kutokana na mazozo wa maji na ardhi ya malisho kati ya jamii hizo za wafugaji ambapo sasa yamegeuka kuwa machafuko.

Haijaekwa wazi nini kimechangia machafuko haya ya hivi punde katika eneo hilo la White Nile.

Shirika la habari la serikali limeripoti kuwa watu kumi na sita waliofairiki walitoka katika pande zote hasimu, idadi kubwa ya wengine wakiwa wamejeruhiwa, nyumba kadhaa pia zikiwa zimechomwa moto.

Machafuko mengine yaliotajwa kuwa mabaya zaidi yalishuhudiwa katika jimbo jirani la Blue Nile, kati ya kabila la Hausa dhidi ya makundi mengine ambapo watu karibia 200 waliuawa katika kipindi cha siku mbili.

Kabila la Hausa ambalo ndilo kubwa zaidi nchini Sudan limekuwa likisema kuwa linabaguliwa pamoja na kuzuiwa kumiliki ardhi katika eneo la Blue Nile.

Kati ya mwezi Julai na mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana , karibia watu 149 waliuawa wengine 65,000 wakipoteza makazoi yao katika jimbo hilo la Blue Nile kwa mujibu wa umoja wa mataifa .

Mapigano haya yanakuja wakati huu ambapo vita vinaendelea kushuhudiwa katika jiji la Khartoum na miji mingine, watu 750 wakithibitishwa kuawaua maelfu yaw engine wakitoroka makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.