Pata taarifa kuu

Malawi : Mtu mmoja afariki huku wengine 23 hawajulikani walipo baada ya boti lao kugongwa na kiboko

NAIROBI – Watu karibia 23 hawajulikani walipo ya kiboko kugonga boti lililokuwa linawasafirisha na kuzama kwenye Mto Shire katika eneo la Nsanje kusini mwa Malawi.

Karibia Watu 20 hawajulikani wlipo baada ya boti walilokuwa wakisafiria kugongwa na kiboko na kuzama kusini mwa Malawi
Karibia Watu 20 hawajulikani wlipo baada ya boti walilokuwa wakisafiria kugongwa na kiboko na kuzama kusini mwa Malawi © Malawi Broadcasting Corporation
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu ofisa wa ngazi ya juu katika eneo hilo la Nsanje, Robert Nayeja, boti hilo lilikuwa likiwasafirisha watu 37 waliokuwa wanaelekea kwenye mashamba yao upande wa Msumbiji, tukio ambalo limethibitishwa na televisheni ya taifa hilo MBC.

Mamlaka katika eneo hilo imethibitisha kuopolewa kwa mwili wa mtoto mchanga, ambaye alikuwa miongoni mwa wasafiri waliokuwa kwenye boti hilo.

Hadi sasa watu 13 wameokolewa wakati huu ambapo maofisa wa polisi wameiabia VOA kwamba idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka wakati huu vitengo vya uokozi vikwa mbioni kuendelea kuwatafuta watu waliozama.

Haya yanajiri wakati huu pia mbunge katika eneo husika akisema kuwa mto huo una mamba na viboko wengi na maboti yanayoendeshwa pale huwa sio maboti yanayotumia injini.

Hii ni ajali ya tatu ya boti kutokea katika mto huo katika kipindi cha miaka miwili.

Tukio hili linakuja ikiwa imepita miezi miwili baada ya watu 511 kuuawaua katika kimbunga kilichoshudiwa nchini Malawi wengine 533 wakiripotiwa kutoweka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.