Pata taarifa kuu

Utekelezaji kamilifu wa mkataba wa biashara huria barani Afrika utaleta mafanikio: IMF

NAIROBI – Ripoti mpya ya shirika la fedha duniani, IMF, inaonesha kuwa utekelezaji kamilifu wa mkataba wa biashara huria barani Afrika maarufu kama, AfCFTA, utaleta manufaa makubwa ya kipato na ajira mpya miongoni mwa mambo mengine

IMFinaonesha kuwa utekelezaji kamilifu wa mkataba wa biashara huria barani Afrika maarufu kama, AFCFTA, utaleta manufaa makubwa  ya kipato na ajira mpya
IMFinaonesha kuwa utekelezaji kamilifu wa mkataba wa biashara huria barani Afrika maarufu kama, AFCFTA, utaleta manufaa makubwa ya kipato na ajira mpya REUTERS - JOHANNES CHRISTO
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake iliyochapishwa mwishoni mwa juma hili, iliangazia namna mkataba huu utarahisisha na kuhuisha ufanyaji biashara hasa wakati huu ambapo dunia inashuhudia athari kadhaa kama ya mabadiliko ya tabia nchi, mizozo, ukuaji wa teknolojia na ongezeko la idadi ya watu.

IMF inasema mageuzi ya kina pamoja na utekelezaji wa mkataba wa biashara huria, kutaongeza wastani wa biashara kwa biadhaa kati ya nchi za Afrika kwa zaidi ya asilimia 53 na mataifa mengine kwa asilimia 15.

Aidha ripoti hiyo yenye kurasa 63, imeongeza kuwa hali hii itasaidia kuongezeka kwa pato ghafi la nchi wanachama kwa zaidi ya asilimia 10, huku wakati huohuo umasikini utapungua.

Waandishi wa ripoti hii wamesema fursa hizi ili zioneshe matunda, zitahitaji uwekezaji wa miundombinu, mitaji ya watu na mazingira mazuri ya kibiashara kwa sekta binafsi ili ikue.

Mkataba wa AfCFTA ulizunduliwa rasmi mwaka 2019 lakini hadi leo bado haujaanza kutekelezwa huku baadhi ya nchi zikiwa hazijauridhia kikamilifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.