Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Côte d'Ivoire: Uchaguzi wa serikali za mitaa na magavana kufanyika Septemba 2

Uchaguzi wa magavana na serikali za mitaa nchini Côte d'Ivoire, mwafaka uliofikiwa kati ya serikali na upinzani kwa ajili ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2025, utafanyika Septemba 2, msemaji wa serikali Amadou Coulibaly ametangaza siku ya Jumatano.

Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara (katikati), Makamu wa Rais Tiemoko Meyliet Kone (wa pili kushoto), Waziri Mkuu Patrick Achi (kushoto), Rais wa Bunge la Seneti Jeannot Ahoussou Kouadio (wa pili kulia), na Spika wa Baraza la Bunge Adama Bictogo (kulia) huko Yamoussoukro mnamo Aprili. 19, 2022.
Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara (katikati), Makamu wa Rais Tiemoko Meyliet Kone (wa pili kushoto), Waziri Mkuu Patrick Achi (kushoto), Rais wa Bunge la Seneti Jeannot Ahoussou Kouadio (wa pili kulia), na Spika wa Baraza la Bunge Adama Bictogo (kulia) huko Yamoussoukro mnamo Aprili. 19, 2022. © AFP / SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Tarehe hiyo imewekwa na agizo la kirais kwa pendekezo la Tume Huru ya Uchaguzi (CEI), amesema. Wanachama 11 wa serikali watawania katika uchaguzi wa magavana, kulingana na orodha iliyochapishwa na Rally of Houphouëtists for Democracy and Peace (RHDP), chama tawala.

Waziri Mkuu Patrick Achi atakuwa mgombea kwenye nafasi ya mwenyekiti wa baraza la madiwani katika kanda ya Mé (kusini-mashariki), jimbo ambalo anatoka. Mawaziri wengine walioteuliwa ni pamoja na Téné Birahima Ouattara (Ulinzi), Kobenan Kouassi Adjoumani (Kilimo), Anne Ouloto (Utumishi wa Umma), Bruno Koné (Ujenzi), Mamadou Touré (Vijana) na Pierre Dimba (Afya).

Rais wa Seneti Jeannot Ahoussou Kouadio na mpinzani wa zamani Mabri Toikeusse, aliyejiunga na chama cha RHDP, pia watawania katika uchaguzi huo. Uchaguzi wa magavana utawezesha kupata mabaraza 31 mapya nchini Côte d'Ivoire. Miaka mitano iliyopita, RHDP ilishinda majimbo 18 dhidi ya 6 yaliyochukuliwa na Chama cha PDCI, chama kikuu cha upinzani.

Uchaguzi huu utafanya uwezekano wa kutathmini nguvu za kisiasa nchini Côte d'Ivoire kabla ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2025. Huu utakuwa uchaguzi wa kwanza kwa chama cha PPA-CI, kilichoundwa na rais wa zamani Laurent Gbagbo muda mfupi baada ya kurejea Abidjan mnamo mwezi Juni 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.