Pata taarifa kuu

Mali: Wasuluhishi wa Kimataifa wataka kufufuliwa kwa mkataba wa amani

NAIROBI – Nchini Mali, tangu mwezi Desemba mwaka uliopita makundi yenye silaha Kaskazini mwa nchi hiyo, yaliyotia saini mkataba wa amani na serikali ya Bamako, jijini Algiers mwaka 2015, yamekuwa yakitangaza kujiondoa kwenye makubaliano hayo, kwa kile wanachosema hakuna utashi wa kisiasa.

Ramani ya Mali
Ramani ya Mali © FMM
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa wiki iliyopita, wasuluhishi wa Kimataifa, wakiongozwa na Algeria na wawakilishi kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, walianzisha tena mchakato wa mazungumzo ya amani.

Wasuluhishi hao tayari wametoa mapendekezo kwa serikali ya Mali na waasi hao wa zamani, yanayolenga kufufua mkataba huo wa amani, lakini hawakuweka wazi, ni mambo gani wanataka pande zote zianze kuzingatia.

Suala tata ambalo linalonekana kuzua mvutano mkali kati ya serikali na makundi hayo yenye silaha ni namna ua kuunda upya jeshi la  nchi hiyo.

Aidha, ripoti zinasema wasuluhishi hao wanataka pande zote zikianze operesheni ya kuyahimiza makundi yenye silaha, kuziweka chini silaha wanazomiliki.

Jitihada hizi zinakuja baada ya wiki iliyopita waasi hao wa zamani kuishtumu seriali kwa uchokozi kwa kupitisha ndege zake za kivita katika ngome zake, kinyume na makubaliano ya amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.